IBRAHIM ROJALA
Member
- Jul 16, 2021
- 25
- 25
Juni 2020 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo muswada wa sheria ya kuwapa kinga viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais na makamu wake,Jaji Mkuu pamoja na Spika na naibu wake ambao ilielezwa kwamba hawapswi kushtakiwa wakiwa madarakani na badala yake atashtakiwa mwanasheria mkuu wa serikali!
Muswada huu ulipitishwa katika kipindi ambacho nchi ilikuwa chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano ya hayati Dkt.John Pombe Magufuli na ni katika kipindi cha utawala huo ambapo kulikuwa na kelele nyingi kutoka kwa wanaharakati mbalimbali juu ya utekelezwaji wa kile kilichoitwa miradi ya kimkakati wilayani Chato Mkoani Geita alikozaliwa Magufuli.
Katika kipindi kifupi cha utawala wa Serikali ya awamu ya tano kati ya Novemba 2015 hadi machi 2021 miradi mikubwa zaidi ya 20 ilikuwa ikitekelezwa wilayani Chato ambayo mingi ilikuwa ikilalamikiwa kukiuka taratibu za kisheria katika uidhinishwaji wake pamoja na upatikanaji wa fedha za utekelezaji wake.
Tutazame baadhi ya miradi hiyo kama mfano wa kielelzo cha uwepo wa makosa ambayo ni nguvu ya kikatiba na kisheria pekee ambayo ingeweza kuweka mzahania katika idhinisho la utekelezaji wake wilayani Chato.
Baadhi ya miradi iliyotekelezawa katika kipindi kifupi cha utawala wa serikali ya awamu ya tano wilayani Chato ni pamoja na hospitali ya rufaa ya kanda ya Chato ambayo ujenzi wake ulianza Septemba 18 mwaka 2017 kwa gharama ya shilingi bilioni 30 iliyojengwa kwa lengo la kuhudumia mikoa ya kanda ya ziwa.
Hoja kubwa kuhusiana na hospitali hii yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 700-1000 kwa siku ni kwamba ilikuwa sahihi kuijenga wilayani badala ya kuijenga katika eneo ambalo ingekuwa rahisi zaidi kufikiwa na walengwa kama ilivyo kwa hospitali nyingine za kanda zilizo katika mikoa iliyoendelea na panapofikika kwa urahisi na walengwa?
Mradi mwingine ni ujenzi wa hoteli ya kisasa yenye hadhi ya nyota tatu katika eneo la Rubabangwe wilayani Chato kwa gharama ya Bilioni 11.04 ulioanza kutekelezwa April 4, 2020 kwaajili ya kuhudumia watalii wanaozuru hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato ambayo ni ya nne kwa ukubwa nchini ikiwa na kilomita za Mraba 4707.
Tatizo kubwa katika mradi huu ni kuwa hoteli hii ilijengwa katika eneo tofauti kulingana na jografia ya hifadhi ya Burigi Chato ambayo kwa asilimia kubwa inapatikana Mkoani Kagera na si wilayani Chato pia ujenzi wake kusuasua licha ya fedha kutolewa kwa wakati na serikali.
Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Mkoa wilaya ya Chato ni mradi mwingine ulioibua maswali kadhaa kutokana na jingo lenye hadhi ya mkoa kujengwa wilayani ilhali majengo mengi ya shirika hilo katika mikoa mbalimbali yakiwa hayana hadhi ya jengo hili na yameendelea kutoa huduma kwa wateja wengi kuliko Chato,Mradi huu uligharimu kiasi cha shilingi bilioni nne hadi kukamilika kwake.
Chato iliendelea kula mema ya nchi kwa kupatiwa mradi wa kituo cha Mabasi makubwa na madogo ya abiria kwa gharama ya bilioni 6.39 kupitia kampuni ya Mayanga Construction katika mkoa ambao kituo kikuu cha mabasi cha mkoa hakina hadhi hata ya kuwa cha wialaya lakini mradi mkubwa ulipelekwa wilayani Chato.
Mnada wa kimataifa wa Buzirayombo uliotekelezwa kwa gharama ya bilioni 4.8 ambazo hazikuwa sehemu ya bajeti ya wizara ya mifugo pamoja na mradi wa viumbehai Rubabangwe uliogharimu bilioni 3.07 ikaendelea kuifanya wilaya ya Chato kupelekwa kimkakati zaidi ili kufanikisha azma ya kuifanya kuwa mkoa.
Mradi mkubwa zaidi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mradi unaweza kuwa umeweka historia ya kugharimu kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuliko miradi mingine ya kimkakati katika wilaya hiyo.
Mnamo Agosti 31, 2016 wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ilisaini mkataba wa Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato na Kampuni ya Mayanga Contractors Limited ya jijini Mwanza ili kuanza rasmi kwa ujenzi wa uwanja huo.
Uwanja wa ndege Chato una urefu wa kilomita tatu ukiwa unalingana na wa Mwanza na una hadhi ya 4C, ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 100-200 zinaweza kuutumia,utekelezaji wa mradi huu awali ulitarajiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 39 kabla ya baadae gharama kuongezeka hadi kufikia kiasi cha bilioni 58.
Kiasi pekee cha wazi cha fedha kinachofahamika kuwa kilipitishwa na Bunge kwaajili ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa uwanja huo zilikuwa ni bilioni mbili pekee,baada ya hapo mengi yalifuata mpaka pale ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali ya mwaka 2020|2021 ilipobainisha kuwa gharama za ujenzi wa uwanja huo zilizidi bajeti.
Ripoti hiyo ilidadavua zaidi kuwa kiasi cha shilingi bilioni 3.62 zilichukuliwa kutoka katika miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya fedha zake kutoka lakini hilo halikufanyika hivyo kupelekea miradi mingine kukwama.
Licha ya mradi wa uwanja wa ndege Chato kukamilika na kuanza kutumika mwaka 2019 hakuna uwazi wa moja kwa moja juu ya mchango wake kwa pato la taifa huku baadhi ya huduma kama vile maduka,huduma za kifedha na migahawa zikiwa ni za kusuasua kwa wasafiri.
Uwanja huu mpya ndani ya kipindi kifupi tatari unahitaji marekebisho kama alivyonukuliwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Geita, Japherson Nnko Aprili 23 mwaka huu akisema wanatarajia kuuboresha zaidi uwanja wa ndege wa Chato ikiwa ni pamoja na kufungwa taa za kuongozea ndege na uzio wa kuzunguka uwanja mzima hapa kuna swali kwamba katika bajeti ya ujenzi wake vitu hivi havikujumuishwa?
Miradi ya aina hii haijawahi kushuhudiwa Butiama Nyumbani kwa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Kivure alikozaliwa Mzee Ali Hassan Mwinyi,wala Msoga kwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kwanini ilikuwa Chato pekee tena kwa kasi kubwa kuliko miradi mingine?
Utaratibu wa utekelezwaji wa miradi ya serikali ni kuwa lazima ipitie bungeni na kupitishwa na bunge kabla ya utekelezaji wake lakini kwa miradi mingi ya Chato haikuwa hivyo.
Mzunguko wa bajeti za utekelezaji wa miradi iliyoitwa kuwa ni ya kimkakati wilayani Chato bila shaka haukukidhi takwa la kisheria linalotaka kuonesha maandalizi ya bajeti katika mradiau miradi husika,uidhinishaji,utekelezaji,usimamizi na utoaji wa taarifa kuhusiana na miradi husika kama inavyoeleza sheria ya bajeti ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika mwaka 2015.
Ukweli mchungu ni kwamba hata kama miradi iliyotekelezwa Chato ilikuwa na malengo ya kuleta maendeleo katika wilaya husika inaacha maswali mengi kuliko majibu juu ya namna ya kuitenganisha na nguvu ya madaraka ya Rais katika kuamua mambo na ulinzi amabo kama nchi tunaupata kupitia katiba ili kudhibiti nguvu hii.
Hapa ndipo takwa la katiba kupaswa kuwa wazi kuwa watu wote wanapaswa kuwa sawa chini ya sheria bila ya kujali kuwa wako madarakani au la,kumshtaki mwanasheria mkuu wa serikali kwa kosa la mtu binafsi kwa makosa binafsi ni mkanganyiko na hili linapaswa kurekebishwa kupitia katiba ambayo ni sheria mama kwa maslahi mapana ya Taifa.

Hatupaswi kusubiri hadi viongozi watoke madarakani kama ilivyokuwa kwa Marais wa Zamani wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Park Geuin Hye wa Korea Kusini,Lula Da Silva wa Brazil Mengitsu Haile Mariam wa Ethiopia ama Mohamed Morsi wa Misri bila kumsahau Frederick Chiluba wa Zambia,Hosni Mubarak wa Misri na wengine wengi.
Katiba mpya inahitajika kwakuwa si kila wakati tutabarikiwa kupata viongozi wenye busaara au wenye hofu ya Mungu lakini tukiwa na katiba imara tunaweza kuwa salama zaidi sisi na vizazi vijavyo pia hakuna na maana yeyote kusubiri kiongozi aliyefanya ubadhirifu wa mali za umma,wanaotajwa kila wakati na ripoti za CAG kuingizia hasara serikali wakitamba mitaani atoke madarakani ndipo ashtakiwe ilhali katika nchi hiyo hiyo vibaka na wadokozi wakiishia gerezani.Hao wote walisubiriwa mpaka pale walipotoka madarakani ndipo wakawajibishwa wa makosa waliyoyafanya wakiwa viongozi,hapa ndipo katiba inapaswa kuwa wazi zaidi ili viongozi wawajibishwe kwa makosa yao katika wakati ambao wameyatenda kama ilivyo kwa wahalifu wengine.
Upvote
4