Miradi ya maendeleo (hususan majengo) wilayani Songwe ipo chini ya kiwango. Tamisemi chukueni hatua stahiki

Miradi ya maendeleo (hususan majengo) wilayani Songwe ipo chini ya kiwango. Tamisemi chukueni hatua stahiki

Songwe Yetu

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
84
Reaction score
99
Wilaya songwe bado imeendelea na maajabu yake. Wasimamizi waliofanya vibaya mpaka inatia kinyaaa bado mkurugenzi anawabembeleza. Kuna sehemu tulipita wakati tunakagua tukaaacha maelekezo wafanye marekebisho kwani ujenzi ulikuwa chini ya kiwango warekebishe madirisha, milango na madawati lakini kwa bahati mbaya marekebisho hayo hayajafanyika tuliporudi kukagua tena sasa sijajua tatizo nini?

Mkurugenzi chukua tahadhari kwa waliosimamia majengo ikumbukwe Rais wetu anatafuta hela kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sio za kula watu. Sasa hivi wanawahonga watu wa halmashauri ili majengo yapokelewe hususani injia wa wilaya. Kuna baadhi ya majengo hayajakamilika na mengine hayapokelewa wakati mda wa kukabidhi umeshapita. Kuta zimepakaliwa rangi bila kupiga msasa madawati mabovu na madirisha mabovu majengo yananyufa kabla hayajaanza kutumia

Naonmba TAMISEMI na WIZARA YA ELIMU iimulike wilaya hii upande wa majengo hususani ya zahanati na mashule yanayojengwa, yapo chini ya kiwango Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wapo tuu ofisini. Tamisemi iwachukulie hatua kwa kushindwa kusimamia maendeleo katika wilaya hii.
 
Ten Percentage

Ndiyo Hovyo Ded Na Mkandarasi Wamekula Kwa Urefu Wa Kamba
Ngoma Ikilia Sana Haichelewi Kupasuka
 
Ten Percentage

Ndiyo Hovyo Ded Na Mkandarasi Wamekula Kwa Urefu Wa Kamba
Ngoma Ikilia Sana Haichelewi Kupasuka
Tunapita kukagua tena nadhani inaweza kuwa wiki ijayo nasikia wamegoma kufanya marekebisho kuna sehemu ye kasema watapokea hivyo hiyvo amesema wenyewe watachoma mafuta mpaka wakome mimi sifanyi marekebisho yoyote.
 
Madiwani si wapo?Madiwani si ni CCm tu,si mliona ndy maendeleo yatapaaa, sasa mnalia nini tena humu? Sasa hivi informer hawapo kwenye maharimashauri, wapo wenyewe kuanzia mkurugenzi mpaka diwani!halafu eti kuna uwizi. Nanii wanasimamia uwizi?
 
Back
Top Bottom