Miradi ya maji 17 Chemba (Dodoma) ni kichomi, hadithi isiyokamilika, bajeti ilipitishwa tangu Mwaka 2020/21

Miradi ya maji 17 Chemba (Dodoma) ni kichomi, hadithi isiyokamilika, bajeti ilipitishwa tangu Mwaka 2020/21

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
Mbunge wa Chemba, Mohammed Moni ameuliza Swali leo bungeni ambapo amelalamikia asilimia 80 ya miradi ya Maji haijakamilika akiitaja miradi hiyo kwa idadi Isiyopungua 17, Mbunge huyu wa Chemba amesema miradi hiyo kushindwa kwake kukamilika kwa kipindi kirefu kutokana na ukosefu wa fedha hali inayosababisha ukosefu maji safi na salama wilaya ya chemba

Aidha, aliongeza kuwa katika Bunge la Bajeti la 2020/21 bunge lilipitisha bajeti ya uchimbwaji wa visima 11 katika wilaya ya hiyo, ambapo mpaka sasa vimechimbwa visima vitatu ambapo alitaka kujua lini serikali itamaliza visima 8 vilivyobakia

Akijibu swali ilo naibu waziri wa maji Andrea Mathew Kundo alikili kuwa miradi hiyo imesimama kutokana ucheleweshwaji wa fedha za wakandarasi ambapo amesema serikali ipo mbioni kutoa malipo ya kiasi cha shilingi bilioni ma moja na arobaini, na uku hati za madai zikiendelea kukusanywa kutoka kwa wakandarasi wanadai

Kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo nchini kwa sasa imekuwa ni tatizo kubwa na sababu kubwa ikiwa ni wakandarasi kutokulipwa pesa za ujenzi wa miradi, maswali ya kujiuliza ni ipo baadhi ya miradi inafadhiliwa na wahisani serikali itujibu pesa za wahisani zipo wapi je hawajatoa na kwanini hawajatoa kama walivyoaidi,

Kukwama kwa miradi ya maendeleo nchini ni dalili ya kukosekana uwajibikaji matumizi mabaya ya fedha au ndio tabia ya kuhamisha fedha na kubadilisha matumizi

Serikali lazima iwajibike kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana
 
Serikali haina fedha, ila Boeing Dreamliner mpya ya ATCL imembeba mheshimiwa Rais akiwa na Katibu wake Waziri Salum na marafiki zake kuhudhuria kongamano la kilimo Marekani. Hivyo ndo vipaumbele kwa sasa.
 
Back
Top Bottom