SoC01 Miradi ya nyumba nafuu za kiutamaduni na kiasilia itaimarisha utalii na pato kwa shirika la nyumba na real estates companies na Taifa kwa ujumla.

SoC01 Miradi ya nyumba nafuu za kiutamaduni na kiasilia itaimarisha utalii na pato kwa shirika la nyumba na real estates companies na Taifa kwa ujumla.

Stories of Change - 2021 Competition

Impimpi

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2019
Posts
466
Reaction score
964
Sio siri kuwa miradi mingi ya nyumba za makazi na biashara hushindwa kuliteka soko kwa Watanzania wengi hasa wa kipato cha chini na badala yake nyumba nyingi zimebaki tupu bila wapangaji ama wamiliki ( wanunuzi) kwani miradi hio hukosa uhalisia wa maisha ya watu wa chini.

Makampuni hudhani kuwa tabaka la kati ( middle class) ni kubwa kufikia kubuni miradi ya nyumba zenye hadhi na gharama kubwa ilhali uhalisia haupo hivyo bali watu wenye maisha ya chini na kawaida ndio wateja wazuri endapo watabuni miradi jumuishi ya nyumba za makazi.

Mathalani ni ngumu mno kwa mtu wa kipato cha chini kupangisha nyumba za miradi hio kwa sababu kadha wa kadha mfano kodi kubwa, umbali wa miradi hio ilipo na huduma muhimu kama shule ,afya na usalama. Wengi huishia kuishi kwenye nyumba uswahilini palipo na huduma muhimu japokuwa hakujapangwa ila angalau mtu atajikimu kulingana na kipato kidogo alichonacho.

Katika masoko ( marketing) kuna kitu kinaitwa marketing segmentation ambapo ni kitendo cha kulivunjavunja soko kulingana na mahitaji tofauti ya wateja mfano vitu kama saikolojia ya mteja , pato la wateja ,tabia , utamaduni na mtindo wa maisha ni vya muhimu sana katika biashara na hiki ndio msingi wa bandiko langu.

KITU MUHIMU CHA KUFANYA

Shirika la nyumba ama makampuni ya real estates waandae miradi ya nyumba za kiutamaduni na hapa napendekeza waunde SWAHILI CITY PROJECT yenye households 1000 ambayo itajengwa mwambao wa bahari ya Hindi mfano Dar es salaam , Tanga ama Zanzibar.

MAPENDEKEZO

1.Mradi ujengwe katika eneo lililopimwa na kufanyiwa utafiti wa kutosha

2. Shirika la nyumba na wataalam wake, Baraza la sanaa Tanzania, Taasisi ya ukuzaji Kiswahili , Wanahistoria na wadau wengine wa utalii na mambo kale wakae pamoja waplan na kubuni mradi huu kwa kuangalia vitu gani viwekwe katika mji vitakavyovutia watalii lakini pia vitakavyovutia wateja katika nyumba hizo

3.Ujenzi uzingatie Swahili Architecture na Swahili local building materials

4.Kuwe na huduma muhimu za kijamii kama shule, hospitali, Maji, Umeme, barabara na uwepo wa vyombo vya ulinzi na usalama.

5.Kuwe na vituo vya sanaa na utamaduni wa mswahili kama ngoma na sanaa nyingine za maonesho.

6.Kuwe na vyakula na mavazi ya mswahili na tamaduni nyingine za Mtanzania ili kukuza kipato cha wakazi wa mji huo na kuvutia utalii.

7.Kuwe na matamasha ya utamaduni mara kwa mara kukuza sanaa na utalii.

8.Wasanii wetu wa muziki wafanye video zao katika mji huu ili kuutangaza kimataifa pia wizara ya sanaa na utamaduni ishawishi wasanii wa Hollywood kufanya filamu zao katika mji huu ili kuutangaza.

FAIDA ZA MRADI HUU

1. Nyumba zitauzika haraka sana na pia kupata wapangaji wengi hivyo kumlipa mwekezaji
2.Pato la mkazi na Taifa kwa ujumla litakuwa kutokana na shughuli za utalii zitakazokuwa zinafanyika
3.Mradi huu utakuwa mfano kwa miradi mingine kama hii maeneo mengine Tanzania katika kukuza utalii.

HITIMISHO
Serikali kupitia shirika la nyumba na makampuni ya upangishaji na uuzaji nyumba yaangalie unafuu wa gharama za upangishaji na uuzaji wa nyumba zilizopo katika miradi yao ili kuendana na hali halisi ya kipato na maisha ya Watanzania ili kuleta tija katika miradi hio.
 
Upvote 0
Karibuni kwa michango wadau
 
Back
Top Bottom