Wanajamvi naombeni Ushauri kuhusu taratibu za kufungua Mirathi,nimepewa jukumu la kuwa msimamizi wa Mirathi ya Shemeji yangu ambaye alikuwa mwajiriwa na kuna mali alizopata baada ya mauti ya mumewe ambaye ni kaka yangu. Je, inawezekana kufungua Mirathi ya mwanamke ukizingatia walioana na ndoa inatambulika kisheria? Mali za Marehemu Kaka yangu zishafunguliwa Mirathi.Huyu Shemeji yangu ana mtoto mmoja wa kike ambaye kwa mujibu wa vikao vya familia ndiye MRITHI wa mali za mama yake.
Zingatia: Marehemu kaka alikuwa na wake wawili,mmoja marehemu mwingine yuko hai na alimjengea kila mmoja wa wake zake nyumba ya kuishi inayojitegemea.
Zingatia: Marehemu kaka alikuwa na wake wawili,mmoja marehemu mwingine yuko hai na alimjengea kila mmoja wa wake zake nyumba ya kuishi inayojitegemea.