Mtoto wa nje ya ndoa harithi kitu, vitu vyake vyoteeee anatakiwa apewe na baba au mama mzazi kabla hajafa ampe kabisaa viwe vyake full stop. Haijalishi ni dini gani, hata serikali pia haitampa kitu labda tu kama wazazi wameandikia kwenye urithi wao. na bado itakuwa ni ngumu.
Kama ni mwanao ndiye hakurithishwa isikupe taabu, mpeleke mtoto wako shule akasome aelimike atapata kazi na siku moja atapata mali zake mwenyewe nyingiiiii kuliko hata hizo za kuachiwa na mzazi wake, hazina mpango sana. Mimi mwenyewe baba yangu alipokufa sikupewa kitu hata kimoja sababu ni mtoto wa nje, na sasa nina elimu,afya nzur,i pesa, kazi na mengineyo mengi tu, naishi raha msitarehe kuliko watoto wa kwenye ndoa, hao waliorithi wakiniona wanajibeba hawana kitu nimewapita woteeeeee!!!!
Usitegee mali za kurithi ukipewa sawa ukikosa tafuta chako na uweke mambo yako sawa.
Ila pia jamani wanaume waache kuzaa zaa ovyo ovyooo inawapa shida sana watoto maisha yamekuwa magumu sana.