Misaada kwa yeyote mwenye uelewe wa mbolea ya kunyunyizia aka booster

Misaada kwa yeyote mwenye uelewe wa mbolea ya kunyunyizia aka booster

Mr simple M

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2020
Posts
2,202
Reaction score
4,653
Naomba kufahamishwa je naweza kuendelea kupiga booster ata baada ya mahindi kutoa mbelewele na je kuna madhara yeyote katika matumizi ya booster natanguliza shukurani
 
Naomba kufahamishwa je naweza kuendelea kupiga booster ata baada ya mahindi kutoa mbelewele na je kuna madhara yeyote katika matumizi ya booster natanguliza shukurani
Unaweza endelea kupiga hasa booster zenye potassium(k) kiasi kikubwa kwenye mchanganuo wa N. P. K mfano 10:7:35.

Hakuna madhara yoyote endapo kipimo kitazingatiwa. Lakini kwa mahindi(na mazao mengine), booster inatakiwa kuwa kama msaidizi tu wa mbolea ya kawaida. Majani hayana mfumo mzuri wa kupitisha virutubisho kulinganisha na mizizi na hasa kwa vile vitatu vya msingi nitrojen, potassium na phosphorus. Vile vinavyohitajika kwa kiasi kidogo sana kama zinc, magnesium n.k ndivyo ambavyo vinaweza kuletwa na booster katika mmea.

Hivyo usitegemee sana booster, mbolea za kawaida tu zinaweza kuleta matokeo mazuri zaidi.
 
Back
Top Bottom