Misaada ya Marekani na uhuru wetu kama Taifa

Hovyo kabisa, yaani ZZK na kachama kake kamfukoni walishafilisika si leo
 
mleta uzi kwa taarifa yako sheria ma katiba inafuatwa kwa jnsi ccm wanavyoona wao. ni mambo mengi tumeyapigia kelele lakini kwa kuwa hayana maslahi kwa ccm basi hayatekelezwi. Ngoja US iingilie kati kwa kusimamisha misaada. Hili la kisitisha misaada wangalau litakigeuza ccm kuheshimu sheria na katiba.

Kuna kujigamba eti tutajitegemea ili tuendelee!! Kwa hiyo tulingoja tunyimwe misaada ndio tujitambue!? Hii kadhia imeletwa na ccm na wala sio suala la nchi huru, kwa hiyo kinachoendelea ni matokeo ya chama kulazimisha kuongoza kwa mabavu. Usidhani hao wamerekani wataishia tu na hiyo MCC, watabana kila mahali. Leteni huo ujuaji kama wa Mugabe leo hii nchi nzima ya Zimbabwe wanaisoma namba. Halafu mleta uzi hii post tako ni ya kujipendekeza kwa ccm wakati wanakiuka sheria na katiba waziwazi.
 
Swali kujiuliza je hizo sababu walizotoa ni kwa manufaa yetu watanzania au yao!!??
 
Subirini mziki wa EU ndio mtawajuwa wazungu wakikupiga counter attack lazima ukae, yani watu mnaotegemea tumbiri kama resources leo mnawaletea jeuri watawala wa Dunia? Halafu hiyohiyo miviongozi ya ccm na familia zao saa hizi iko bize kucheza green card rottary wakija kwenye Tv wanadanya wananchi wakati wao wanatamani leo kesho wapate uraia wa Marekani.
 
Na bomba la mafuta lipite kenya ili ccm wajue walichofanya si kizuri
 
mahakaman hawakutakiwa kwenda kupinga matokeo ya urais, bali kupinga kufutwa kwa uchaguzi.
Mahakama zipi? Mahakama hizi ambazo Jaji mkuu ana kadi ya ccm na anakwenda kuomba kuteuliwa na ccm kugombea urais? Wewe ni total mental case. Mipumbavu kama wewe iliyojazana kwenye vyama ndio imesababisha nisiwe mwanachama wa chama chochote.
 
nchi yetu huru na ina mifumo yake, na kwa vyovyote vile kadhia kama hii ina jawabu lake katika mfumo. hatuwez kupata jawabu kwa vitisho vya misaada.
"Nchi yetu ina Mifumo yake" mawazo ya hivyo kabisa hayo.
Matumizi ya silaha zo moto na vikosi vya majeshi dhidi ya raia ndiyo majawabu ya hizo kadhia!!!
 
Nchi imegawanyika kisiasa kutokana na figisu za ccm, kujitegemea kwa % 100 haitowezekana. Haki ndio itakayoleta umoja na maendeleo ya kasi.
 
kama marekani wanaheshimu utawala wa sheria wangeliwashauri cuf kushiriki uchaguzi badala ya kususia. kwanza misaada gani ya wamarekani..mtu anakupa shs 5000 mkono huu anachukua shs 200000 mkono mwingine. hasira yao ni kuona jinsi awamu ya 5 ilivyodhamiria kupambana na ufisadi na unyonyaji. bila ufisadi mikataba ya kuchuna mtu ngozi kama ile ya iptl, richmond, songas, agreco haiwezekani. nchi sasa inapambana na vibwanyenye uchwara vinavyofaidika na ubeberu wa marekani na wanyonyaji wote duniani.
 
Kama mtanzania naamini 100% nchi yetu hasa sisi watanzania hatuko huru. na hata mihimili iliyopo sio huru.
nchi inaongozwa kwa kiburi tu cha watu wanoadhani wao ni zaidi ya raia wa nchi hii.

Hakuna mahali unaweza kuipata haki kama ya uchaguzi hasa kwa Zanzibar kupitia mahakama zetu. Jitengeni na Dunia kwa kiburi cha kutaka kuibakiza ccm madarakani tuone wapi tutafika!!!!

Msaada wa mcc ni muhimu maana ndio uliokuwa unapeleka umeme vijijini kupitia REA, leo hii Kinampanda haitapata umeme kwa sababu za uchaguzi wa zanzibar ambao ccm hawtaki kukubali kushindwa. Ni maeneo mangapi hayatapata maji? Au tumeingiwa kiburi na ujeuri kisa wizara ya fedha inakuja na siasa za eti tunakusanya kodi kwa kiwango kikubwa nje na mallengo??? Acha tuone miaka mitano hii kama hio kodi ya wamachinga itaendesha nchi!
 
kama maogezi katika meza yalishindikana unafikiri suluhisho lilikuwa ni nini? unajua kwanini watumishi wa Ubolozi SA wamerudishwa muulize Maalim alifanya nini nao wenzie wamerudishwa, kwanini haendi na wenzie kwenye mazungumzo anaenda mwenyewe? jiulize kabla hujahoji , je sheria inasema nini hali ikiwa hivyo.
 
nchi yetu huru na ina mifumo yake, na kwa vyovyote vile kadhia kama hii ina jawabu lake katika mfumo. hatuwez kupata jawabu kwa vitisho vya misaada.

Dotto;
Ungeacha mambo ya kitoto ukajikalia kimya ingelikufaa. Unasema nche yetu ina mifumo, hivyo umeona mifumo hiyo ya kuwaachia kundi moja ijifurahishe kwa mifumo waliojitungia mibovu ndo MCC wawanenepeshe?? Hiyo mifumo haikuwepomkatiba ilivyokuwa ikikanyagwa, kisa kuwafurahisha viongozi? Mifumo hiyo haikuwepo Rasimu ya Warioba ikitupwa kando watu wakajilambia mamilioni ya fedha na wengine kupewa vyeo kwa kujua kutukana kwenye lile BMK?
Kweli mahaba niue yana taab. Nasema Hongera Marekani kutunyima na kufutilia mbali hata jina letu kupokea msaada huo wa MCC.
Kwanza, karibu zaidi ya nusu ya huo msaada ilikuwa inawapa kitambi viongozi wachache. Waache wale hizi za tra zitawatosha wakipungukiwa wale maescro mengine watakayo buni.
 
Mahakama zipi? Mahakama hizi ambazo Jaji mkuu ana kadi ya ccm na anakwenda kuomba kuteuliwa na ccm kugombea urais? Wewe ni total mental case. Mipumbavu kama wewe iliyojazana kwenye vyama ndio imesababisha nisiwe mwanachama wa chama chochote.
Duh! Hii ngumi ya uso hasa, kapigwa jamaa nadhani kaomba na maji kabisa. Kuna watu lazima waambiwe ukweli in hardway
 
Hapa hatuongei kama taifa na CCM wasilazimishe hivyo! Waelewe kuwa wao wanaongea kama chama chao cha CCM kisha wanatuhadaa na blah blah za kuvaa koti la uzalendo ambalo ni la kihuni ili tuonekane wamoja katika hili. Sisi tunasema kuwa hatupo tayari.

CCM waelewe kuwa haya yanayotokea sasa ni matokeo ya uhuni wao na si vinginevyo. Hivyo wasituhusishe sisi. Sisi kwa dhati kabisa tunaunga mkono maamuzi ya wanajamii wa MCC kutokana na sababu za msingi kabisa walizotoa. Kwa hili huo ndiyo uamuzi na msimamo wetu thabiti na tunausema bila kupepesa.Tunamueleza kila mwana CCM!
 
hio ni nonsense mkuu kwasababu hata kule burundi nkuruzinza alisema burundi ni huru haipaswi kuingiliwa kwenye maamuz yake...pia mahakam ya katiba ilimpa go ahead nkuruzinza kugombea tena japokuwa wote tunajua haikuwa sawa kwahio kama wewe kwako unaona right basi usijue kwamba na jumuiya za kimataifa znaona right...eti uhuru? uhuru kufanyiana dhulma ndo uhuru wewe? naona chama chenu kinawatuma sana cku hizi kuja kutetea ushetan mlioufanya zenji
 
..Ebo!! nilikuwa namsoma huku nashangaa huyu jamaa mbona anapingana na tamko la chama chao,kumbe...!!!
 
 

Well said, comrade. Hata mimi sikubaliani sana na kilichotokea Zanzibar ingawa kiuhalisia na CUF nao walifanya hovyo kimkakati. Hili la mtandao nalikubali kwa sababu mitandao inatumika vibaya, sisi tulikuwa holela mno. Lakini kinachonikasirisha ni hawa Wamarekani kuja na masharti ya kikoloni wakati nchi nyingine kama Saudi Arabia na nchi kadhaa za kiarabu ikiwemo Misri hawafanyi hivyo. Marekani ni taifa la hovyo, la kibabe kama ilivyokuwa kwa Roman Empire nyakati hizo. Hapo ni lazima tukae chini na kuukataa ujinga wao wa demokrasia ya upande mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…