mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
Anandika Khamis Kagasheki.
Ninaona usumbufu wa kufunga barabara na kusimamisha magari unazidi kuwa mkubwa. Ukiuliza unajibiwa "msafara." Tatizo hili limekuwa likiongezeka lakini kwa sasa limekuwa kero hapa Dar es Salaam.
Tarehe 7 July 1963 (Saba Saba Day) katika kilele cha cha sherehe za kuzaliwa TANU, Baba wa Taifa alihutubia Taifa kuhusu "Mbwembwe."
Tarehe 13 July 1963, Mwalimu aliwaandikia mawaziri wake wote na makatibu wakuu wote akiwaonya kuhusu jambo hilo la "mbwembwe." Kuhusu "police escorts" Mwalimu aliandika, "kabla hatujaingia serikalini kulikuwa na utulivu barabarani, lakini baada ya kuingia serikalini, hatuendi popote bila police escort." Aliendelea, " zipo nyakati escort inahitajika" na akailenga kwa Rais na Makamu wa Rais/Waziri Mkuu. Akaendelea kuandika, "the President of Tanganyika is fast becoming the worst public nuisance the City of Dar es Salaam has ever to put up with! Whenever he decides to out, whether to a dinner, a dance, or even to visit some friends, the normal flow of traffic has now to be interfered with...it is rapidly becoming impossible for anybody in Dar es Salaam to guess how long it will take him to drive from A to point B..." Hii ilikuwa 1963.
Leo asubuhi (Alkhamis) barabara nyingi maeneo ya Oysterbay zilikuwa zimefungwa na magari kusimamishwa kwa zaidi ya dakika 25. Pia naona wapo maaskari wanaokwenda mbali zaidi kwa kusimamisha baadhi wa raia.
Jana (Jumatano) barabara ya Ali Hassan Mwinyi (mida ya kuanzia saa kumi/kumi na moja) magari yamesimamishwa zaidi ya dakika 20. Sijui kama ilikuwa msafara au traffic officer.
Uslama wa viongozi wetu ni kipaumbele muhimu lakini tuzingatie humu barabarani sio wagonjwa wote husafiri kwa ambulance kwa maana ya ving'ora. Humu barabarani wamo watu wagonjwa, watu wazima wanaokabiliwa na changamoto nyingi za kiafya. Bahati mbaya wapo maofariki ndani ya magari wakipelekwa hospitali.
Escorts zimekuwa nyingi barabarani. Sitaki kutoa judgment lakini naomba sana mtazame ni watu gani wanastahili privilege hii.
Soma Pia: Wananchi wa Korogwe tunakereka kusimamishwa muda mrefu barabarani ili kupisha misafara ya viongozi wa Siasa, hii sio sawa
Barabara zetu ni kila kitu kwetu. Kufunga barabara dakika 20 au nusu au zaidi, uchumi wa taifa unaathirika kwa kiasi gani? Appointments za watu mbali mbali zina athirika kiasi gani.
Kuandika haya simfundishi mtu yeyote kazi yake lakini ninakumbusha tu.
Kazi njema.