Misafara ya Viongozi wakati huu ni kama misafara ya wafanyabiashara binafsi

Misafara ya Viongozi wakati huu ni kama misafara ya wafanyabiashara binafsi

Izy_Name

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2020
Posts
772
Reaction score
1,733
Nikikumbuka miaka ya nyuma kuanzia kwa Kikwete na Magufuli hali ni tofauti na sasa. Watu hawana tena shahuku ya kujipanga barabarani kushuhudia msafara kama enzi zilizo pita hapo nyuma kidogo kwa sasa Rais anapita lakini ni kama kapita Alikiba tu ingawa hawakosekani raia wa kushangaa barabarani ila kwa kiasi kikubwa kuna utofauti mkubwa na kipindi cha nyuma.

Wakati mwingine unawaza lbd ni kwasababu ya maendeleo ya utandawazi lkn bado hoja haina mashiko maana haiwezi kuwa ghafla namna hiyo.

Baadae nikahisi lbd na viongozi wamelitambua hilo ndio maana mikutano yao ya mikoani wana ambatana na escort kubwa ya mabasi yaliyobeba wanafunzi na watu wa vijijini wengi kama umeshawahi kushuhudia utakuwa shahidi kwenye mikutano na hadhara ya ccm malanyingi panakuwapo na sura nyingi ngeni na haziendani kabisa na wakazi wa maeneo hayo vile vile malanyingi kunakuwa na nguvu ya wasanii na watu maarufu kwa nyuma.

Baada ya hapo watu hawazungumzii tena alichosema kiongozi ila utasikia mala Diamond aliimba kdg tu nk.

SWALI.
Je, siasa na viongozi wa kisiasa especially watawala wamekosa mvuto na ushawishi kwa raia ama watu wapo serious zaidi na maisha?

NB: Mimi sio muumini na shabiki wa misafara mirefu ya viongozi kwani inatumia gharama kubwa zisizo na msingi.

Pia soma: KERO - Misafara imekua kero, Raia wanazuiwa muda mrefu kupisha misafara
 
Back
Top Bottom