Misamiati iliyoko kutokana na watu au bidhaa

Misamiati iliyoko kutokana na watu au bidhaa

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
1. Kisado -- Bidhaa ni rangi ya nyumba, ya kampuni ya Sadolin. Walikuwa wakiweka kwenye makopo ya ukubwa fulani yaliyopachikwa jina la "visadolini" au "visado".

2. Kimbweta - Kiti na meza cha zege, mara nyingi huwapo kwenye taasisi za elimu ya juu. Vilibuniwa na Prof. Mbwette. Wengine huviita Vimbwete.

3. Wekundu wa Msimbazi -- Timu ya Simba Sc. ilianza kutamkwa hivyo na Isaac Muyenjwa Gamba, alipokuwa mtangazaji katika kipindi cha michezo cha redio moja hapa nchini.

4. Ongezea misemo mingine tafadhali.
 
Kihiyo-- mtu anaye danganya kuhusu taaluma asiyokuwa nayo, ilitokana na aliyewahi kuwa Mbunge wa Temeke marehemu Kihiyo alipoanganya kuwa ana shahada ya uhandishi kumbe ni Fundi Mchundo mwenye cheti cha VETA
 
Bukta..kaptula (kampuni ya vifaa vya michezo ya zamani ya bukta)
Sheli..haihitaji maelezo ya ziada
Biki...kampuni ya kalamu maarufu ya Bic
Shatafu...mpira wa usafi wa chooni kutoka kampuni ya Shataff
Kiwi..nayo haihitaji maelezo
Pampasi..nayo haihitaji maelezo
Blubendi...kutokana na blue band brand
 
Kilaza.....hutumika kumuelezea mtu asiye na akili za darasani au asiyejua kitu, ilitumika sana pale chuo kikuu cha Dar (UDSM), inatokana na mwanamuziki wa zamani marehemu Juma Kilaza, akifananishwa kuwa hajui kitu kwa kumlinganisha na mwenzie Mbaraka Mwinshehe wote hawa walitokea Morogoro!
 
Chai-Maharage--- hili lilitumika sana kwa magari ya usafiri hasa Dar na miji kama Mwanza, lilitumika kuelezea namna watu walivyokuwa wanakaa kwa kutizamana ndani ya gari, mengi ya haya magari yalikuwa hayana siti kama siku hizi ila kulikuwa na mabenchi tu upande wa kulia na kushoto hivyo watu walilazimika kukaa kwa kutizamana kama wako kwa mama lishe..ndio asili ya neno chai-maharage
 
Back
Top Bottom