Haggle => Kubishana kwa ajili ya bei ya bidhaa
I know they will haggle over the price of tomatoes. => Najua watabishana kwa ajili ya bei ya nyanya.
Slump => Kushuka kwa ghafla
I am worried that the Microsoft stock will slump. => Nina wasiwasi kwamba hisa ya Microsoft itashuka bei.
If he falls asleep he will slump over in his chair. => Akilala atainama chini kitini kwake.
Pampa => Wanda wa bara la Marekani kusini. Neno hili latumika nadra sana. Labda unamaanisha "pamper"?
I travelled for three days to cross one pampa of Argentina. => Nilisafiri kwa siku tatu nivuke wanda mmoja wa Argentina.
Humper => Bible Humper ni mtu ajaribuye kukulazimisha kuwa Mkristo. Matumizi tofauti ya "humper" ni lugha mbaya ya mitaa.
That Bible humper tried to force me to be baptized. => Huyu mhubiri mwenye nguvu alijaribu kunilazimisha kubatizwa.
Temper => Tabia (nomino) au kupunguza (kitenzi)
(nomino) I lost my temper when he stole my bicycle. => Nilihamaki alipoiba baisikeli yangu.
He can't control his temper. => Hawezi kudhibiti tabia yake mbaya.
(kitenzi) You should temper your anger before speaking to your mother. => Uipunguze hasira yako kabla ya hujasemea mama yako.
Abide => Kuzingatia au kufuata
If you abide by the rules you will be benefitted. => Ukifuata masharti utanufaika.
Baadhi ya haya ni maneno magumu. Labda fafanuzi zangu za Kiswahili ni mbaya, lakini mifano ya Kiingereza ni mizuri.