Misamiati mipya ya Kiswahili sanifu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kuna haja ya kujulishana misamiati mipya ya lugha yetu adhimu. Kila siku lugha yetu inakua na misamiati inaongezeka kila siku.

Hapa kuna baadhi ya misamiati, pia naomba ndugu zangu muongezee baadhi ya maneno ya Kiswahili sanifu.

Tafrija mchapalo -cocktail party.
Kanguvuke - jenereta
Rununu - simu ya mkononi
Weledi - profesionalism
baobonya - keyboard
Puku - mouse.
Ngamizi - kompyuta
Wavuti - internet
Tovuti - website
Kichakata matini - word processor
Runinga - television.

Naomba tuongezee misamiati mingine
 


Masuala mtambuka-cross-cutting issues
 
non renewable resources - vyanzo visivyo jadidifu,
Kuperembwa - to be monitored,
Photosynthesis process - mchakato wa usanisisuru
 
Asante Mkuu
 
hapa kwa kichakata matini kuna haja ya kufikiri upya, dah!
kweli kabisa mkuu tunaweza kufanya vyema kuliko "Kichakata matini" hata kwenye simu "rununu" nayo sidhani kama inafaa aliyekuja na haya maneno inabidi asishirikishwe tena kwenye hii issue
 
Deficit= Nakisi
Decentralisation= Ugatuzi
Feedback= Mrejesho
Strategic Plan= Mpango mkakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…