Misamiati mipya ya Kiswahili sanifu

wale wazee wa baraza la kiswahili wanaharibu sana hii lugha ya kiswahili
 
Hang over-mning‘inio wa juu,
Feedback-mlisho wa nyuma!
 
Kanzi - data
kibugi - virus
kinzarusi - antivirus
kilawa - output as in computers
KiSaKi [KIhuluku SAdifu cha KIjenetiki] - gmo i.e genetically modified organism
rimokonto, kisengeretua, kiungambali, kitenzambali - remote
sakura, vinjari - surf
amilisha - booting
ufuru - sms
scanner iitweje?
 

Baobonye (Keyboard) ya kawaida kwa mfumo wa Marekani

Bodimama (Motherboard)



Bongo kuu (kompyuta) (CPU)

Mobile Phone kibolo



Kiendeshi diski kuu (Hard disk driver)

[TABLE="class: infobox, width: 1"]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Puku (kompyuta) (Mose)

RAM
(kumbukumbu isiyo na mpangilio maalumu).




Tarakilishi


Kompyuta ya kisasa (kwa Kiingereza personal computer au PC) :
  1. Kiwamba (skrini)
  2. Bao kuu
  3. CPU (bongo kuu)
  4. RAM (Kumbukumbu ya muda)
  5. Kadi za nyongeza kama vile kadi mchoro n.k.
  6. Ugawi wa umeme
  7. Kiendeshi CD
  8. Kiendeshi diski kuu (HDD - kumbukumbu)
  9. Baobonye
  10. Puku


Nywila au neno la siri (Password)

[h=1]Virusi za kompyuta
[/h]
Virusi za Kompyuta ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaa ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle. Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara. Virusi zinasambaa kwa njia ya intaneti lakini pia kwa njia ya sidii au diski yoyote ya kubebea data kati ya kompyuta. Virusi vinaweza kuharibu mafaili na kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kompyuta yako.


 
Nashukuru kwa mchango wako. Mobile phone = kibolo kwa misingi gani?
nimependezwa na bodimama=motherboad
nashuku cpu kuitwa bongo kuu. ile dhana ya processing hupotea tusemapo bongo kuu. Kwangu ni SEKU {SEhemu Kuu ya Uchakataji} au KIKIU {kitengo kikuu cha uchakataji}
 
diga kosotu = hard disc
diski mweko = flash disc
diski tepetevu = soft disc
diski gandamize = floppy disc
gwagula = computer wizard
kitingishi = vibrator
 
Jamani, mnasemaje "geopolitics" na "to update" kwa Kiswahili? "jiosiasa" na "kusasisha"?
Asanteni
 

Watoto UMADI ni street children
 
Watoto UMADI ni street children

Street children si Watoto wa mtaani?

"Umadi" ni nini?
Nani anatumia "watoto umadi"?

Je, misamiati hii ni ya mtindopeke ("idiolect", yaani lugha ya mtu binafsi) au lugha ya mitaani au lugha sanifu?

Tafadhali mnisaidie kuelewa.
 


MINGINE

Kurunzi ni Torch
Kikutakona ni Round about
Kingamuzi ni Antena
Ueledi ni Ujuzi au ujuvi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…