Hilo huntha [Khuntha] ninalitumia katika mazungumzo ya kawaida
[Serikali mahututi].....sidhani kama ni Kiswahili sanifu
Serikali mahututi ni hii iliyopo madarakani!
In the first place, kuna shida gani na neno SERIKALI YA MSETO? mbona ni clear?Hilo laweza kuwa kweli.
Lakini serikali mahututi haiwezi kutumika kama mbadala wa serikali ya mseto kama ilivyoanishwa na mtoa mada
Katika gazeti la RAI la Jana (09/08/2012) katika maoni kulikuwa na misamiati mipya ya kiswahili. Misamiati hiyo ni:
WanaJF nimeona niwaletee misamiati hiyo ili muanze kuitumia kwa nia ya kukienzi Kiswahili chetu. Erotica kwa vile siku hizi kisu imekuwa njia maarufu ya kujifungua, ukitoa katika chumba cha upasuaji utapelekwa Sadaruki (usiseme ICU).
- ICU (intesive care unit) = SADARUKI.
- Serikali ya Mseto (coalition government) = SERIKALI MAHUTUTI.
- Viumbe vyenye JINSI zote mbili (Me na Ke) = HUNTHA (wingi ni mahuntha)
Ndimi Bazazi!
Hilo laweza kuwa kweli.
Lakini serikali mahututi haiwezi kutumika kama mbadala wa serikali ya mseto kama ilivyoanishwa na mtoa mada
Nimeipenda hiyo SADARUKI
Halafu 'mahuluti' wala si msamiati mpya. Ni kwamba tu huwa halitumiki sana.
Viumbe vyenye JINSI zote mbili (Me na Ke) = HUNTHA (wingi ni mahuntha)
In the first place, kuna shida gani na neno SERIKALI YA MSETO? mbona ni clear?
Mi naona kuna maneno yanayohitaji zaidi kiswahili kama CPU, REDIO,GARI, BAISKELI etc!
Nasikia wenzetu Wanigeria walipooma baiskeli kwa mara ya kwanza waliita "Iron Horse"!.. at least inaleta sense!
Hongera kwa kuendeleza Lugha ya kiswahili,lakini neno SERIKALI MAHUTUTIsioni mantiki ya kutumika kama mbadala ya neno SERIKALI YA MSETO.
Siyo serikali "mahututi". Ni serikali "mahuluti". Kama waliandika serikali 'mahututi' basi walikosea tu tahajia kwa sababu "mahututi" na "mahuluti" tahajia zake zimepishana herufi moja tu.
Kwa hiyo serikali "mahuluti" ni Kiswahili sanifu kabisa.
Katika maneno hayo mawili, 'mahututi' na 'mahuluti', fonimu 't' na 'l' ni mofimu kwa sababu ndizo zilizosababisha tofauti ya maana. Ni muhimu sana, kwa mantiki hiyo basi, kila mara tunapoandika msamiati tujiridhishe na otografia husika kuepusha uwezekano wa kupotosha wafuatiliaji wa nyuzi zetu. Hata hivyo tunamshukuru mleta uzi na mchango ulioutoa kwa wanajamvi wengine.Siyo serikali "mahututi". Ni serikali "mahuluti". Kama waliandika serikali 'mahututi' basi walikosea tu tahajia kwa sababu "mahututi" na "mahuluti" tahajia zake zimepishana herufi moja tu.
Kwa hiyo serikali "mahuluti" ni Kiswahili sanifu kabisa.
Katika maneno hayo mawili, 'mahututi' na 'mahuluti', fonimu 't' na 'l' ni mofimu kwa sababu ndizo zilizosababisha tofauti ya maana. Ni muhimu sana, kwa mantiki hiyo basi, kila mara tunapoandika msamiati tujiridhishe na otografia husika kuepusha uwezekano wa kupotosha wafuatiliaji wa nyuzi zetu. Hata hivyo tunamshukuru mleta uzi na mchango ulioutoa kwa wanajamvi wengine.
Nyani Ngabu nakuhakikishia kuwa sikupata kiwi ya macho kiasi cha kutoelewa mchango wako kuntu juu ya mada iliyoko jamvini. Ukisoma michango ya wachangiaji wengine ni lazima utamaizi nililolisema.Sijakuelewa hata kidogo. Ni nani kapotosha wafuatiliaji wa nyuzi hapa?