Misanya Dismas Bingi.

Madodi

Senior Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
176
Reaction score
59
habari zenu wana JF..naombeni mnijuze huyu jamaa aliyejipatiaga umaarufu enzi zile akiwa Radio One kupitia kipindi cha Chemsha Bongo, yuko wapi sasa..maana ni muda mrefu sana sijamsikia.
 
yah ni mwalimu ndugu wa somo la sosholojia!
 
habari zenu wana JF..naombeni mnijuze huyu jamaa aliyejipatiaga umaarufu enzi zile akiwa Radio One kupitia kipindi cha Chemsha Bongo, yuko wapi sasa..maana ni muda mrefu sana sijamsikia.
Alipata nafasi ya kusoma UDSM kazini kwake wakamnyima ruhusa chuo kilipofunguliwa akaomba likizo na kuripoti chuo. Huku nyuma wakamfukuza kazi!.

Pale UDSM jamaa ni kichwa mbaya, akafumua 1st class hivyo kuajiriwa na chuo direct kama Tutorial Asst huku akiwa na full sponsorship ya masters akamaliza na kuwa lecture hapo hapo akaunganisha na Phd anamaliza this June, Mwezi November anavishwa Ph.D yake na kubadili jina kwa kuitwa Dr. Misanya Dismass Bingi ( B.A. ...Hons. UDSM, M.A .... UDSM, Ph.D ...UDSM) Senior Lecture then Assc Prof na baada ya miaka michache atakuwa ni
Prof. Misanya Dismass Bingi!.

Pasco
 
Pasco umeuuuuuuwa ngoja na mimi nikaze msuli nimalizie kadiploma kangu
 
Pasco unamjua vizuri sana,we ndio pasco mayalla? Maana nae alikua fani kama yako!! Nani aliyezui asiende kusoma? Joyce au mengi? Da Misanya yupo juu sana kichwa cha mzumbe hicho
 
Kudadadadadadadekiiiiiiiiii... Pasco umenikuna...
jamaa ni mshikaji wangu, enzi akiwa media, tulipenda kunywa, kujirusha na kufuatilia kwa kutafuta mambo flani ya goodtime. Mwenzetu katuacha mbali hata yale mambo fulani hatafuti tena!, sasa yeye sio mtu wa kutafuta tena bali sasa yeye ndio mtu wa kutafutwa!. Mpaka anawakimbia!.

Yuko juu mbaya!.
 
Pasco unamjua vizuri sana,we ndio pasco mayalla? Maana nae alikua fani kama yako!! Nani aliyezui asiende kusoma? Joyce au mengi? Da Misanya yupo juu sana kichwa cha mzumbe hicho
Mkuu King Kong, Mimi ni Pasco wa jf, ila huyu jamaa namjua yeye ni Pascal Mayalla, Joyce ndie mkewe aliishia zake Marekani Pascal akajirudia zake bongo. Mimi Pasco ni memba humu jf na Pascal Mayalla nae pia ni memba wa jf!.

Ila pia humu jf haturuhusiwi kumfananisha memba na mtu yoyote wa ukweli hata kama unamdhania yeye ni fulani, hilo ni kosa linaitwa name calling na adhabu yake huwa ni ban!.

Pasco
 

thanx mdau wang
 

Vipi P. Mayalla na Misanya Bingi , wanafahamiana?
 

jamaa kumbe sio level yetu tena
 
Wanafahamiana sana! na mimi nawafahamu wote wawili.

Wanafanana fanana... Wote ni watanashati,na wote ni wanandoa, na nadhani wote kwenye ndoa zao,kumekuwa na kunyemelewa na mwovu ibilisi...
 

Ok mkuu pasco wa jf,kumbe joyce muhaville ni mke wa misanya bingi?
 
misanya hakupokea vibahasha kama wafanyavyo kina pasco siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…