Misemo na Methali za Kiswahili

Mr. Miela

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2007
Posts
1,254
Reaction score
2,121
Wajameni;

kuna mtu anaweza kunipa link itakayonisaidia kupata Misemo ya kiswahili katika mtandao?
 
wantala chikokoto, chaulezi chinyunyunyu..................
 
Hapa kuna methali za kiswahili

Kuna kazi kibao za Kiswahili kwenye wikipedia and its sisters.


Ebwana methali nyingine nilidhani nafahamu maana zake. Hii inatoka wikiquote,
Usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe.
Don't trust a fool with your private matters, if you do, you will be the fool!​


.
 
Mchelea mwana kulia....?
 
...kwamba mzazi asipomuadabisha mwanae, atakuja kulia yeye?

Mmepatia vema nyote wawili:

Kila msemo wa kiswahili una maana sana! Nawapa kwa kifupi ili mmalizie na wengine mjaribu kupambanua kwa undani zaidi.

Wale mnaoendekeza wanenu gharama yake kwenu ni kubwa. Methali hiyo inaendana kabisa na "Samaki mkunje angali mbichi"... Sambamba naweza kusema inaendana kabisa na "Maji yakimwagika hayazoleki!"

Kuna huu pia:-

Mficha uchi.............
 

.... hazai!
 
wantala chikokoto, chaulezi chinyunyunyu..................

Gang, samahani hivi hayo yako katika Kiswahili au ni lugha nyingine tu asilia?!
Naomba tafsri yake tafadhali iwe Kiswahili au lugha nyingineyo yoyote.. thanks.
 



...kwamba mzazi asipomuadabisha mwanae, atakuja kulia yeye?

... msemo huu una apply kwa vijibwa pia... kwamba usipo kaadabisha kajibwa, kitakuhangaisha kikikua na kuwa jibwa!! 😀


where u bn fool?! missed ya.
 
Mficha uchi.............
....hazaizai ovyo.

Unajua, Invisible, huu msemo, ni wanaume wamejitungia wapate kujisadia kwa kupumbaza wanawake.

Ukiwa nje ya ndoa na ukawa unaficha basi hutazaliana zaliana nje ya ndoa, kitu ambacho ni kizuri kwa mficha.

Ukiwa ndani ya ndoa na ukawa unaficha ina maana hutaki kuzaa tokea hapo. Kitu ambacho ni nia ya mficha.

Kama nakosea, hebu nisaidie kama ujumbe "mficha uchi hazai" una mantiki au ujumbe kwa manufaa ya mficha.
 
Mficha uchi.............



Unadhani mtunzi alilenga kumaanisha kama inavyoelezwa hapa chini?

Literal Meaning: We should let our friends know our troubles so they can help us, even if that involves revealing something shameful.
 
Mimi huwa nazimia sana methali hii:

Mgaagaa na upwa (mpwa?)............

Hivi hii misemo inaungukia kwenye kitabu cha methali pia?
- Dunia tambara bovu
- Utakiona cha mtema kuni
 
Dunia tambara bovu; na Kukiona cha mtema kuni
Hizi ni nahau siyo methali.
 
Mficha uchi....
Hii methali inaendana na methali hii:
Mficha maradhi kifo kitamuumbuwa au Mzaa mzaa mwishowe utumbuka usaha.

"Samaki mkunje angali mbichi..."
Hakisha kauka hakunjiki

Mgaagaa na upwa...
Hali wali mkavu

Dunia tambara bovu
Dunia ni sawa na nguo chakavu, inataka taadhari sana jinsi ya kuishi na kusabiiana na watu. Bila ya taadhari inaweza kukufika maafa au kupata hasara... ni sawa na mtu aliye vaa nguo iliyo chakaa... wakati wowote inaweza kumchanikia.

Utakiona cha mtema kuni
Hii methali inatokana na hadithi au simulizi ya mkata kuni (Mtema kuni... Hiki ni kiswahili cha zamani). Kwa ufupi inasimuliwa kwamba mkata kuni alikwenda porini kwa nia ya kutema kuni (kukata kuni) kutokana na sababu anazo zijuwa yeye au kwa kuzidiwa na mawazo alipofika porini akapitiwa na usingizi (kama bado nakumbuka vizuri) ndio kwanza ulikuwa muda wa Mawio yaani jua linachomoza). Alipokurupuka... kuangaza huku na huku shoka halioni, na hali anakumbuka vizuri kulichukuwa...

Yeye hakahisi labda limedondoka mahali... akaanza kulitafuta kuanzia Mawio mpaka Machweo (Kuzama kwa jua Wakati wa Magharibi) Mwisowe akajikuta amechoka na shoka halionekani. Akaamua kukaa chini ya mti ili apumzishe akili na kutafakari upya wapi alipolidondosha shoka lake. Wakati anajiandaa kukaa chini kuangalia begani kwake analiona shoka lake... kumbe alikuwa amesahau kuwa shoka lilikuwa amelining'iniza begani kwake...

Hapo ndipo palipo patikana huo msemo wa "Utakiona cha mtema kuni... Kutafuta shoka wakati lipo begani."

Hii kidogo inataka kufanana ule msemo wa "Utakiona kilicho vunja shoka mpini ukabaki... msemo huu umetokana na simulizi za Sir H. Rider Haggard kwenye moja ya simulizi zake zinazo elezea visa vya mwindaji Tembo hodari Bwana Allan Quatermain (Makumazan or Macumazahn)... Na msaidizi wake Msolopaganzi (Umslopogaas) na shoka lake Nkosi kazi (Inkosi-kaas)... Bwana Henry Curtis, na rafikie Kapiteni Good, (Bwana Mzuri).
Kwenye liwaya hii ndipo pia lilipo patikana jina Gagula... Kibibi kilichokuwa kichwawi (Kigagula)

Vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu ambavyo vinaonyesha au kusimulia ujasiri wa hali ya juu sana... Pia kwenye ile riwaya ya Machimbo ya Mfalme Suleiman na nchi ya Wakukuana... Na vile vingine ambavyo havikuwahi kutafsiriwa kwa kiswahili kama vile SHE & Ayesha (Tibet)

Wale walio wahi kusoma watamkumbuka sana Bwana Msolopaganzi (Umslopogaas) na majigambo yake a.k.a Mikwara mizito aliyokuwa akiwatishia maadui zake... Nakumbua mwisho wa riwaya Umsolopaganzi alipomaliza kazi ya kulinda ngazi kuu... Alikuwa amepata majeraha mengi mwilini... akajua kuwa mwisho wa uhai wake umekaribia ndipo alipoamua kufa na shoka lake (Bibi msemi).... lilizungusha shoka lake kiasi ya kuonekana kama mwali wa moto... kisha kwa pigo moja... pigo lililo takatifu... Pigo lililo nyooka... akalishusha shoka lake kwa kasi ya ajabu na kulipasuwa jiwe lile na huku shoka lake likitawanyika vipande vipande na kubakia akiwa ameshikilia mpini wa shoka ukiwa mzima.... Mzee wa kizuru akaanguka chini akakata roho...

Soma baadhi ya vipande toka Riwaya ya Allan Quatermain

Soma majigambo (Mikwara ya mzee wa Kizuru)



Umbopa...
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…