Misemo ya makonda wa Daladala

Misemo ya makonda wa Daladala

Abiria: We konda kuna siti humo?

Konda: Zipo bi mkubwa, choma ndani, unaenda wapi?

Abiria: Magomeni

Konda: Fungua nauli kabisa...........................poapoa, haya rudi nyuma

Abiria: We konda mbona sizioni siti?

Konda: Acha masihara bi mkubwa, hao wenzako wamekalia mawe kwani?
 
Abiria: nishushe hapo hapo mbele

Konda: nani akushushe!,shuka mwenyewe..kwani mi ndo niliyekupandisha?

Hapo tayari kashachukua nauli yake kitambo sana,huwezi kusikia kauli kama hii ikiwa bado hajachukua nauli
 
Back
Top Bottom