Mishahara iongezeke au tudhibiti bei za mafuta

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Wasalaam,

Bei za mafuta zinahusika moja kwa moja na ongezeko la gharama za maisha kutokana na mfumuko wa bei ambapo kuenda sawa na hali hiyo, mishahara hupaswa kuongezwa ili kuwafanya watumishi wasipoteze nguvu ya kununua.

Mishahara ya watumishi wa serikali haijapanda kwa muda wa miaka kadhaa na hivi karibuni Rais amesema 'Lile Jambo lipo' ambapo wanapiga hesabu ili kubaini waongeze asilimia ngapi mishahara ya watumishi. Wakati huohuo bei za mafuta zimeendelea kupanda kwa kasi na kuonesha hali mbaya mbeleni, yaani hata mtumishi akiongezewa mshahara Julai haitakidhi kwa kuwa kasi ya ongezeko la mshahara haliko sawa na kasi ya ongezeko la gharama za maisha.

Hata hivyo, fedha za matumizi mbalimbali zinaweza kutumika ku-subsdize mafuta ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi na tozo ili bei za mafuta ziwe stable. Njia hizi mbili haziwezi kwenda pamoja. Yaani tutachagua kuongeza mishahara ili kumpa nguvu mnunuzi, au kumlipa mnunuzi ili kupunguza gharama anazoingia.

Moja kati ya jambo baya ni kuwa, ni rahisi sana kwa bei za mafuta, lakini kushuka ni suala gumu kidogo.

Swali ni je, tuongeze mishahara ili watumishi wawe na nguvu ya ununuzi, au tusubsdize ili kudhibiti bei za mafuta?

Mkoba Mfuko wa kutoka Morogoro
 
Kama wewe unadai mishahara iongezeke ili bei ya mafuta ibakie pale pale, je! Wafanyabiashara wadogo wadogo unawafikiriaje??
 
Mishahara kuongezeka haipunguzi bei ya mafuta bali inaongeza nguvu ya ununuzi(Purchasing Power) kwa anayelipwa mshahara ili kutoathiri aggregate demand.
 
Sawaa,,najuwa haipunguzi bei ya wese,,ila wenye kipato kidogo kwa maana wenye boda na vigari nani wa kuwatetea!!! Umeegemea upande mmoja kwa waajiriwa,,,

Kwangu mimi namuomba mheshimiwa rais ashushe bei ya mafuta walau 1500 per lita japo ngumu sana.
 
Wasalaam,

Bei za mafuta zinahusika moja kwa moja na ongezeko la gharama za maisha kutokana na mfumuko wa bei ambapo kuenda sawa na hali hiyo, mishahara hupaswa kuongezwa ili kuwafanya watumishi wasipoteze nguvu ya kununua.

Mishahara ya watumishi wa serikali haijapanda kwa muda wa miaka kadhaa na hivi karibuni Rais amesema 'Lile Jambo lipo' ambapo wanapiga hesabu ili kubaini waongeze asilimia ngapi mishahara ya watumishi. Wakati huohuo bei za mafuta zimeendelea kupanda kwa kasi na kuonesha hali mbaya mbeleni, yaani hata mtumishi akiongezewa mshahara Julai haitakidhi kwa kuwa kasi ya ongezeko la mshahara haliko sawa na kasi ya ongezeko la gharama za maisha.

Hata hivyo, fedha za matumizi mbalimbali zinaweza kutumika ku-subsdize mafuta ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi na tozo ili bei za mafuta ziwe stable. Njia hizi mbili haziwezi kwenda pamoja. Yaani tutachagua kuongeza mishahara ili kumpa nguvu mnunuzi, au kumlipa mnunuzi ili kupunguza gharama anazoingia.

Moja kati ya jambo baya ni kuwa, ni rahisi sana kwa bei za mafuta, lakini kushuka ni suala gumu kidogo.

Swali ni je, tuongeze mishahara ili watumishi wawe na nguvu ya ununuzi, au tusubsdize ili kudhibiti bei za mafuta?

Mkoba Mfuko wa kutoka Morogoro
Wewe kati ya watanzania million 60 ni wangapi wanalipwa mishahara na serikali?
 
Uzi upo kwa mfumo wa swali ili tuchague kipi bora, thus nimetaja njia zote ninazofikiria na madhara yake
 
Option ni moja...Matajili kuingia kwenye kundi la wanyonge kutembea kwa mguu...baiskeli ztauzika sana mwaka huu...ila wachawi wajinga sana wanaloga..wanashindwa Kumlogha Putin...?
 
Acha kuwa selfish ndugu, mafuta yanaathari kwa wote, wewe unazungumzia as if hii nchi wafanyakazi tu ndio wenye kustahili kuongezwa mishahara. Kuna watu wengi tu maisha yao hayatokani na mishahara nao wasemeje?
 
Sawaa,,najuwa haipunguzi bei ya wese,,ila wenye kipato kidogo kwa maana wenye boda na vigari nani wa kuwatetea!!! Umeegemea upande mmoja kwa waajiriwa,,,

Kwangu mimi namuomba mheshimiwa rais ashushe bei ya mafuta walau 1500 per lita japo ngumu sana.
Kazi ya kutengeneza asal anaweza nyuki tu, nzi hawez, mafuta 1500 sitasahau ilikuwa,mwaka 2021 Leo tunaongelea sh 3000+ two times. Na bado inazid kupaaa
 
Vyote vifanyike kwa pamoja.mishahara ipande kwani ni hakiya watumishi.pia mfumuko wa Bei uthibitiwe.
 
Back
Top Bottom