Habari wakuu,
Nimekuwa nasumbuliwa sana na mishipa kuvuta na kuuma mpk mguu unacheza cheza kuanzia usawa wa tumbo mkono wa kulia yaani sina raha kabisa. Nimeenda hospitali nikapewa dawa lkn hazinisaidii maumivu hayapoi wala kuisha inafikia hatua hata kutembea vzr nashindwa,yaani ni kuanzia pembeni ya tumbo,paja na mguu wote unacheza cheza yaani hata tako likitisika naumia, mwanzo niliambiwa ni ukosefu wa madini labda lkn baada ya kupima tatizo halikuonekana,naomba kujua chanzo na tiba ya tatizo hili