Kuna siku ilitokea misiba miwili kijijini kwetu na wote walizikwa siku moja. Kaya moja ilikuwa masikini na nyingine wana kiuwezo uwezo. Yaani wananzengo walienda kuzika kule kwa masikini chapuchapu wakaondoka hata bila kumaliza taratibu za kimila wanawahi huku ambako kulikuwa na vyakula vya kutosha na pombe. Waliisimanga sana ile familia masikini kuwa walitimiza wajibu tu lakini huu wa hii familia nyingine ndiyo msiba hasa wenye hadhi. Jambo hili liliniuma sana. Misiba imegeuka kuwa sehemu ya show off na watu wanakuja kula na kunywa. Yaani ukifiwa kama huna milioni kama 5 hivi kazi unayo. Utachekwa mpaka ukome. Wanacheka mpaka aina ya jeneza....
Hakun mtu asiye taka kitu kizuri!! Duniani, km yupo ni taahira!!! hata hao waliofiwa walitamani wajumuike huku kwa tajiri lkn wangesemwa vibaya!!! acha waende tu!!
Asa jamani kwa akili ya kawaida tu na utu!! maskini awape nini ?? huoni wamemsaidia?? hata km ningekuwa mfiwa ningewaruhusu ili wanipunguzie mzigo!! tena huko vijijini wanachangiwaga!!
siyo misiba tu!! jenga mijengo ya maana town, Pata madaraka sirikalini, kama Lowasa masai walijaa Ikulu! pata fedha, Mali za kufa mtu, kula na kusaza, nakwambia ndo utajua una ndugu bwena!! watakuja ndugu hata usiowahi kuwasikia! ni kawaida kwetu sisi waafirika! kazi kwako! sasa
uwafukuze au uwakaribishe!! uwapende au uwachukie! uwapige au uwaache wale msosi!! na watakula hasa na kuosha vyombo!! hawatakoma kuja watakuja tena na tena!! so long as umezaliwa Bongo, na ni mbongo!!
watakulimia bure km una shamba, watasindika miwa bure km una kiwanda, wataosha mabasi bure tena alfajili na mapema km unayo!! wao ili mradi wale tu!! na kuangalia TV! Utawafanya nini??? ukiweza fukuza uone km utapata pesa tena!!
vitakuja vizee vya kila aina na story nyiiingi!! wakikuzoea pia unapigwa chochote kilicho karibu yao!! ! live bila chenga!!! bidae saaana unaombwa msamaha!!! wanakuja tena!! yaani km ni mnoko, sijui mchoyo!! heee utabaki kubweka km umbwa kila siku!
utawafunga, watatoka, wataomba msamaha, lkn hawataacha kuja kamwe hata uende Africa kusini watakuja huko! Ili mradi wewe ni ndg yao! na wana kujua sasa wewe kazi kwako uwafukuze au uwapokee!! uwatukane, uwadharau!! iyo ni wewe sasa lkn wao wamekuja!!
ukiwafukuza watakupachika jina la unoko tu baaaasi!!! ila wao wanaamini msaada ni kwa faida zao!! ila wanao wakipata shida huko mbele watapewa misaada but wataimbiwa jinsi ulivo wafanya wewe baba yao!