Misiba ya watu weusi ni tamthilia tupu!

Misiba ya watu weusi ni tamthilia tupu!

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Misiba yetu huwa ni event fupi yenye mambo mengi ya ajabu, yakuchekesha, kuhudhunisha na kustajaabisha.

Misibani huwa ndio fursa nzuri kwa ajili ya wambea na wanafiki. Wanatunga stori kuhusu kifo na maisha ya familia yenye msiba. Unakuta kuna vikundi vikundi vya wakina mama, vya wakina baba, wengine mchanganyiko kila kikundi kikiwa na stori yake ya chanzo cha kifo cha marehemu. Akifa baba utasikia mama ndio amemuua.

Misibani ndio pesa humwaga nyingi angali marehemu alipokuwa mgonjwa walikuwa wakilia ukata na huku watafuta sifa wakijionesha kufanya vikazi na kutoa michango ili jamii iwaone na wenyewe wamo.

Huku unakuta vijana vugu vugu limeanza kuhusiana na mgawanyo wa mali. Na wale wa uke wenza ndio shida balaa, kila mama anavutia kwake huku mke mkubwa akidai vikubwa kwa maana ndio ameanza ku-hustle na baba na huku mke mdogo akisema kuwa baba amefia kwake na yeye ndio amemuuguza na amemtakia yeye apate vitu fulani na fulani.
 
Na mimba zinatungwa misibani...🙄🙄.

Watu wanapata wapenzi wapya misibani.

Watu wanafanyiana fitina misibani.

Wengine wanafanyiana mambo meusi ya kulogana.

Wengine wanatafuta mwanya wa kupiga hela za michango ya msiba waneemeke.

Full drama, full tamthilia.
 
...ha ha ha safi sana...shughurika na maisha yako uwaachie msiba wao
Kabisa mkuu , kwa sababu nilishatembeza marufuku kuona kenge yoyote inayoitwa mchungaji sijui na mambo yote yanayohusu kanisa kwenye mazishi yangu .

Ngoja nikaushe kweli coz ukifa huna cha kufanya.
 
Back
Top Bottom