Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Msimu ni maneno yasiyo sanifu yanayoanzishwa na kikundi cha watu wachache wenye utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi. Kwa kawaida maneno hayo huzuka na kupotea, ila yale yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha.
Tafiti zimebaini kuwa mitandao ya kijamii imekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza msamiati wa lugha ya Kiswahili kupitia maneno ya misimu. Maneno ya misimu hutumiwa katikamitandao ya kijamii kama alama ya utambuzi na kushirikishwa maarifa miongoni mwa watu wenye utamaduni, umri au akili zinazofanana.
Misimu katika nyanja za kisiasa mabadiliko ya kiutawala yameibua miongoni mwa maneno kama HAPA KAZI TU, MAJIPU, WATUMISHI HEWA, RUKSA, VILAZA, UBINAFSISHAJI NA UTANDAWAZI. Mabadiliko ya kiuchumi yamesababisha kuibuka kwa maneno mbalimbali kama VYUMA VIMEKAZA, KUPAMBANA NA HALI YAKO, JERO, DALA, MAKINIKIA NA BUKU.
Kwa upande wa nyanja za kijamii na kiutamaduni kumeibuka maneno kama CHURA, AMSHA DUDE, JAZA UJAZWE, NA TOA MALINDA. Hata hivyo maneno hayo yakiendelea kutumika kwa muda mrefu katika jamii husanifiwa na kuwa maneno sanifu ya lugha. Miongoni mwa hayo maneno ambayo yameshika mizizi ni SHANGINGI, UJASIRIAMALI, UBINAFSISHAJI na kadhalika.
Katika pitapita zangu kwenye nyuzi za watu humu ndani ya JamiiForums nakutana na misimu ambayo bado haijaingizwa kwenye lugha yetu ya Kiswahili. Lakini inaonekana maneno haya yana nguvu sana na inawezekana yanazungumzwa hata nje ya JamiiForums. Ningependelea kutaja baadhi ya maneno machache: MKUU, BIKO, NJIA KUU, KUDANGA, KIBENTENI, JIWE, KUGEGEDA, PAPUCHI, MALINDA, JIPU, MARIOO, BAHARIA, DUDU, BASHITE, 0713/TIGO, KIBAMIA, MSAMBWANDA, KUPIGA SHOW, MBUNYE, NIKALA MZIGO, PIGA MASHINE, KUPIMA OIL, WAZUNGU/WAJOMBA HAO, GENYE N.K
Andika misimu inayotumika ndani ya JamiiForums (hata katika jamii inayokuzunguka) na maana zake ambayo ungependwa yaingizwe kwenye Lugha ya Kiswahili.