Misimu ya maisha

Misimu ya maisha

Mecury

Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
83
Reaction score
40
Siku nyingine baada ya kula mlo mmoja tu na muda mfupi tu baada ya kuzipitia jumbe fupi za zamani kutoka benki fulani hapa nchini ambayo nami nilikuwa mteja wa muda mrefu sana.

Nikikumbuka miamala niliyokuwa naifanya kwa ajili ya kukidhi mahitaji yangu na starehe mbalimbali.

Nimemkumbuka pia girlfriend wangu wa kipindi kile, ambae kila wakati akitimba geto wadau wanabaki kuulizana MECURY katoa wapi tena chombo hii mtoto alikua hazoeleki kabisa, mpya kila kukicha.

Nimeukumbuka mwili wangu uliokuwa umejengeka vizuri kabisa sababu ya kupata milo kamili na ziada pia, na hilo kupelekea kuwa 'crush' wa mabinti wengi waliopata bahati kunishuhudia katika siku zangu za neema.

Nimekumbuka mavazi maridadi niliyokuwa navaa, hakika sikuwa mtu wa kupitwa na fasheni ya wakati huo.

Mwaka unaelekea wa pili huu sijanunua kitu hata kimoja zaidi ya shati moja tu, nipo single ingawa sio kwa kupenda takribani miezi saba sasa.

Kwakweli siamini kama na leo mimi nimekuwa mtu wa kuishi siku baada ya siku.

Ila najipa moyo na kutumaini siku zangu za neema zitajirudia tena.

Sasa hivi nilichobakiza ni matumaini tu na jitihada ndo kampani yangu. Kila siku nikiomba zinirudishe katika siku zangu za neema.
 
We are sailing in the same boat bro. Let's keep on fighting and praying! All in all pole na jipe moyo, amini yatapita!
 
Mecury,

Mkuu kama umri umeshavuka 40, hiyo ndio wahenga waliita "Fainali Uzeeni". Pole sana maana hata ukija kuzikamata hela saizi kumeshakua jioni hutaweza tena kurudi kwenye hiyo lifestyle na kufanya mambo uliyokua unafanya.
 
Kila matokeo yana sababu zake,huenda ulikuwa mtu wa starehe na kujisahau sana kwamba mambo huwa yanabadilika,kaza buti usimame upya, usikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We are sailing in the same boat bro. Let's keep on fighting and praying! All in all pole na jipe moyo, amini yatapita!
Thanks man, nazidi kupambana na naamini haya ni mapito tu.
 
TheChoji,
Umeongea point sana na hii inanitia moyo niongeze spidi katika juhudi za kupambana nirudi katika hatua nilizo kuwapo mwanzo na ikiwezekana zaidi.

Ingawa bado sijafikia hiyi miaka, lakini umeongea kitu cha msingi sana.

Kwani muda hausubiri mtu.
 
Nina uwakika mleta uzi ni muhitimu wa chuo kikuu na ni muhanga wa ukosefu wa ajira.
 
Karibu mtaani budda, kaza buti, pambana, kulilia na kujichoresha kwa watu hakusaidii kitu.
 
Karibu mtaani budda, kaza buti, pambana, kulilia na kujichoresha kwa watu hakusaidii kitu.
Asee sijamlilia mtu isitoshe sijaomba msaada wa aina yoyote kwa mtu kwenye huu uzi, nilichofanya ni kama therapy flani hivi kupunguza machungu yangu.
 
Mecury, Haupo peke yako, Tupo Wengi tulioporomoka Mkuu, Inafikia Wakati Unajiuliza hivi Mimi ndo Yule Fulani,. Unapigwa Nyege Mpaka Unazikumbuka Mbunye ulizokua unazikwepa Zamani.
Hatari sasa na walivyo na hisia kali za kugundua mfulio wanaweza wakakunusa tu wakajua hamna kitu huyu mtu siku hizi.

Yani hapa mtaani mpaka baadhi ya watu hawaitikii salamu zangu.
 
Kama mawazo yako ni kutaka kuwa na hela ili ufanye starehe,kuwa na mademu wanaojiuza na kuvaa ili watu wakuone hata upewe 1 USD billion kesho tu utakua tena masikini......pole sana kwa kutokua na akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mawazo yako ni kutaka kuwa na hela ili ufanye starehe,kuwa na mademu wanaojiuza na kuvaa ili watu wakuone hata upewe 1 USD billion kesho tu utakua tena masikini......pole sana kwa kutokua na akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kutokua na akili lakini ni makosa ambayo vijana wengi tunapitia, & by the way tunajifunza kupitia kupitia makosa.

Na hongera pia ww mwenye akili ambae hujawahi kufanya makosa maishani mwako.
 
Back
Top Bottom