Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Kwa sasa kama ni kwenye mpira unaweza kusema CHADEMA wamepoteana. Maana hawajui mpira waanzie wapi! Waanzie pembeni nyuma au waanzie mbele. Maana kila hoja wanayoibua imeonekana ni hoja mfu na haiuziki.
Lakini yote ya haya yanayowakuta CHADEMA ni kwa sababu muasisi wa taifa letu Mwl Julius kambarage Nyererea aliacha misingi imara ndani ya mioyo ya Watanzania. Na misingi hiyo ni kuwa wazalendo. Maana taifa huwa linajengwa ndani ya mioyo ya wanananchi wake.
Kwa uzalendo walionao watanzania kila hoja ambayo imekuwa ikiibuliwa na CHADEMA wamekuwa wakiipuuza na kuwaona kuwa hawafai. Mfano walikuja na hoja ya kuwa hivi sasa kinachofanyika ni maendeleo ya vitu na sio watu. Kwa uzalendo wa watanzania, CHADEMA imepuuzwa sana. Maana huwezi kusema ujenzi wa kituo cha afya au barabara sio maendeleo ya watu, maana vinajengwa ili vitumiwe na watu.
Walikuja na hoja ya kipuuzi eti kujenga miundo mbinu,shule na hospital si kitu si chochote. Maana hata mkoloni alijenga. Pia walienda mbali na kudai eti, maendeleo katika sekta hizi hayana maana sababu hivi sasa hakuna uhuru. Maneno haya yamewaudhi sana watanzania wazalendo. Yaani CHADEMA hawajui kuwa mkoloni alikuwa anatunyonya kwa kila kitu? Kuwa alijenga miundo mbinu sehemu ambazo alikuwa na maslahi, kama sehemu ambazo kuna malighafi. Na kuhusu uhuru unaweza kusema hakuna uhuru hapa Tanzania? Watu wanafanya shughuli na kujadili mambo usiku na mchana!
Wamekuja kuona wamebugi wakaja na hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania. Watu wakahoji mtaitekeleza vipi? Wakakosa majibu. Kumbe ilani ya CCM imelitanabaisha hili suala vizuri kabisa na limewekwa wazi namna ambavyo litatekelezwa. Hapo ndio wameishiwa nguvu.
Kuharibu kabisa pale walipowadhalilisha watanzania kuwa nchi hii inalishwa kila kitu na mabeberu. Hili limewakera sana watanzania. Sababu misingi aliyoiacha mwl Nyerere ni kuwa taifa linalojitegemea. Ndio maana ukienda kila kona watanzania wanajishulisha na kilimo,biashara na ufugaji. Na hii imewavunja nguvu CHADEMA maana wananchi wamewapuuza sana. Hata moto walionza nao kwenye kampeni umeanza kufifia.