Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Misingi na kanuni za kilimo bora.
Neno Msingi lina maana ya mwanzo wa kufanya shughuli yeyote inayokusudiwa ili kuweza kufikia malengo. kwa hiyo katika kilimo ipo misingi muhimu ifuatayo:
Kuwa na mipango thabiti inayotekelezeka kabla ya kuanza kufanya kazi yeyote ya maendeleo ni vyema, kuweka mpango kazi ili iwe dira wakati wa utekelezaji. Hivyo wakulima wanatakiwa waweke malengo yao ya kilimo kwa kuangalia Usalama wa chakula na kipato
Mipango bora.
Ni mipango ambayo inamsaidia mkulima kupata chakula cha kutosha na fedha ili kuondokana na umaskini. Mipango inatakiwa iwe shirikishi kwa kuona kuwa wakulima wana shiriki katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia pamoja na kutathmini.
Kuchagua eneo linalofaa kwa kilimo.
Kwa kuwa kilimo ni kazi ya kisayansi, eneo linalofaa kwa kilimo liwe na rutuba, mteremko wa wastani, liwe sehemu inayopitika ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na pembejeo wakati wa uzalishaji.
Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu.
Ni muhimu mkulima kujiwekea kumbukumbu za uzalishaji, mapato na faida ili kupima mafanikio ya kazi yake.
Matumizi ya kanuni za kilimo bora.
Neno kanuni lina maana ya utaratibu wa kisanyansi uliofanyiwa majaribio kwa muda mrefu na ambao umekubalika utumike wakati wa uzalishaji wa mazao.
Kanuni za kilimo bora
• Kutayarisha shamba mapema Kwa kutifua.
• Kupanda mbegu bora kwa nafasi inayostahili.
• Kupunguzia miche na kubakiza inayoshauriwa
• Palilia mapema-si zaidi ya wiki mbili baada ya kuota mazao..Plazi ziwe mbili au zaidi.
• Weka mbolea ya kukuzia mara baada ya palizi.
• Weka dawa ya kuua wadudu wa mimea.
• Linda mazao yako na Wanyama waharibifu Vuna mazao yako baada ya kukomaa vizuri.
• Sindika mazao yako na kuyaweka kwenye mifuko inayoingiza hewa baada ya kuweka dawa.
• Hifadhi mazao mahali pazuri pasipo vuja au kufikiwa na wanyama waharibifu.( Panya)