theriogenology
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 8,748
- 15,681
Utangulizi
Biashara ni utafutaji na usambazaji wa mahitaji ya walaji au watumiaji katiks sehemu mbalimbali.
Ili biashara iendeshwe kwa mafanikio kuna taratibu za kusheria ambazo nilazima zifuatwe. Uendeashaji wa biashara husimamiwa na kanuni mbalimbali. Kanuni hizi humlinda mfanyabiashara na mlaji (mtumiaji) dhidi ya mabadiliko yasiyo ya halali ya bei, matangazo ya uongo, matatizo katika soko, viwango duni vya bidhaa, ajira, uvunjaji wa mikataba, njia potofu za ushindani wa biashara, kudharau bidhaa na kutouza biashara.
Hivyo basi katika kuanzisha biashara kuna mambo muhimu ya kuzingatia baadhi ya mambo hayo ni utafiti..mtaji..elimu ya biashara..fedha na benki.
1. UTAFITI
Katika kufanya biashara yoyote ile ni vizuri kufanya utafiti, matokeo ya utafiti huo yatadhihirisha mambo yafuatayo
a) Kwanza mazingira ya eneo la biashara, mazingira haya yataonesha kuasi cha wakaji, mahitaji yao na bidhaa zinazopendelewa zaidi.
b) Pili kiwango cha ushindani uliopo ushindani huu unaweza kudhihirika kwa wingi wa maduka hayo.
c) Mwisho ni hali ya usafiri, utafiti utaonesha kuwepo aina na gharama za usafiri katika eneo husika. Matokeo ya utafiti yatasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kuanzisha na kuendesha biashara katika eneo husika.
2. MTAJI
Baada ya utafiti kukamilika, hufuatia upatikanaji wa mtaji mfanyabiashara anaweza akaupata mtaji huo kwa njia zifuatazo;
a) Njia ya kwanza ni kujiwekea akiba mwenyewe katika benki kila baada ya muda fulani kiasi kikubwa huweza kupatikana kwa ajili ya kuanzisha biashara.
b) Njia ya pili ni kukopa kutoka benki mtu anaweza pata mkopo wa kuanzishia biashara kutoka kwa benki.
c) Njia ya tatu, kuchanga fedha za mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara ki-ushirika.
d) Njia ya nne na ya mwisho ni kukopa fedha kwa ndugu..rafiki au watu wengine kwa makubaliano maalumu.
3. ELIMU YA BIASHARA
Jambo jingine muhimu ni ufahamu mzuri wa biashara. Ili kuendesha biashara kwa faida ni muhimu mfanyabiashara awe na ujuzi wa kutosha wa kuendesha biashara. Hii ni pamoja na kuwaheshimu wateja wake, kuwa mwepesi kugundua mahitaji sahihi ya wateja wake na kuwa mkweli daima
Vilevile ni muhimu mfanyabiashara awe na ushirikiank mzuri na watu wengine muhimu katika shughuli za biashara na aweze kudumu na kuongoza vyema shughuli za kutunza kumbukumbu muhimu kama vile risiti/stakabadhi...daftari la fedha safu mbili...daftari la mauzo ya mwezi na kutwa...ankara ya mahitaji...daftari la manunuzi ya kutwa na kitabu cha benki cha akiba.