Misingi ya kuishi pamoja

Misingi ya kuishi pamoja

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
1. Ukifika Sehemu... *Salimia*
2. Ukiondoka Sehemu..... *Aga*
3. Ukisaidiwa....... *Shukuru*
4. Ukiahidi...... *Tekeleza*
5. Ukikosea.... *Omba Msamaha*
6. Kama Hujaelewa..... *Uliza*
7. Unacho... *Gawa Kwa Wengine*
8. Huna.... *Usione Donge*
9. Ukivunja.... *Lipa*
10. Kama Hupendi...... *Heshimu*
11. Ukipendwa... *Onesha Upendo*
12. Huwezi Kusaidia... *Usisumbue*
13. Ukiharibu... *Rekebisha*
14. Ukikopa.... *Lipa*
15. Ukiulizwa .... *Jibu*
16. Ukiwasha....... *Zima*
17. Ukifungua...... *Funga*
18. Ukinunua.... *Lipa*
19. Ukichafua.. *Safisha*
20. Ukipungiwa..... *Punga*
21. Ukiazima... *Rudisha*


_Ukizifuata kanuni hizi, utaona jinsi utakavyoishi na watu vizuri hata kama huna hela.
 
Umeongea ukweli asilimia 100 yaani 100%

Jirani yangu kaazima testa yangu ya umeme ili afungie taa zake si akaenda kuivunja akasema ataninunulia nyingine lakini hadi leo kimyaa na nimempotezea tu, na akija kuazima kitu kingine namwambia sina hata kama hicho kitu ninacho.

Ukiharibu=Rekebisha.
 
Back
Top Bottom