Misingi ya kuishi vizuri na watu

Misingi ya kuishi vizuri na watu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
1. Ukifika Sehemu... Salimia
2. Ukiondoka Sehemu..... Aga
3. Ukisaidiwa....... Shukuru
4. Ukiahidi...... Tekeleza
5. Ukikosea.... Omba Msamaha
6. Kama Hujaelewa..... Uliza
7. Unacho... Gawa Kwa Wengine
8. Huna.... Usione Donge
9. Ukivunja.... Lipa
10. Kama Hupendi...... Heshimu
11. Ukipendwa... Onesha Upendo
12. Huwezi Kusaidia... Usisumbue
13. Ukiharibu... Rekebisha
14. Ukikopa.... Lipa
15. Wakikuuliza .... Jibu
16. Ukiwasha....... Zima
17. Ukifungua...... Funga
18. Ukinunua.... Lipa
19. Ukichafua.. Safisha
20. Ukipungiwa..... Punga
21. Ukipewa.... Shukuru
22. Ukiazima... Rudisha

''Ukizifuata kanuni Hizi, Utaona Jinsi Utakavyoishi Na Watu Vizuri Hata Kama Huna Hela, Hii Ni kwa Binadamu Wote Hata Kama Ni Kiongozi'''
 
Hizo kanuni ni kwa upande wa jinsia gani?
 
Iyo namba nane inamuhusu Kamanda Asiyechoka , nyboma na Idugunde the witch
image_search_1642860801093.png
 
Ahsante Kwa muongozo...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
#20 - Inatakiwa iwe ukipungukiwa - punguza hapa na pale, kama tunavyofanya na mshahara
 
Back
Top Bottom