Misingi ya waafrika inafutwa kwa juhudi

Misingi ya waafrika inafutwa kwa juhudi

More problems

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
432
Reaction score
257
Nimekuwa nikiwaza sana Kuhusu suala la dini na kusoma makala mbalimbali humu na sehemu nyingine.
Nilichokuja kuambulia ni kuwa katika matabaka mengi yaliyopo duniani waafrika ndio tabaka lililoweza kukengeuka kwa kiasi kikubwa kutoka katika imani yao asilia.

Kwa kiasi kikubwa tuliletewa kitu kinaitwa ustaarabu kupitia uislam na ukristo.
Chakushangaza ni kwamba wakati wanaeneza walichokiita ustaarabu hawa watu (waarabu na wazungu) hawakuwa na ustaarabu kabisa bali walikuwa wanyanyasaji, waonevu, wezi na walaghai. Na mpaka sasa uhusiano wako na sisi umejengwa katika misingi hiyo, wanatudharau.

Hili limesababisha walio na fikra yakinifu za kuhoji na kutafakari kuwa na wakati mgumu katika kupokea hizi imani zilizoletwa na hawa watu.
 
Back
Top Bottom