Misri, Ethiopia, Sudan zakubaliana matumizi ya Mto Nile

Misri, Ethiopia, Sudan zakubaliana matumizi ya Mto Nile

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Misri, Ethiopia na Sudan wamefikia makubaliano ya awali ya kujaza maji na shughuli nyingine kwenye bwawa kubwa linalojengwa Mto Nile.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi tatu, pamoja na Marekani na Benki ya Dunia, imesema kwamba washiriki wanaojadiliana wamekubaliana kujaza bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia wakati wa msimu mvua kati ya miezi ya Julai na Agosti.

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema lolote kuhusu masuala ya msingi yanayozunguka mgogoro huo ambayo ni kasi ya kujaza bwawa hilo.

Ethiopia inataka kujaza bwawa la Grand Renaissance kwa miaka 6 lakini Misri imependekeza angalau mradi huo uchukue kipindi cha miaka 10 kwa kuhofia kwamba kuchukua kipindi kifupi kutaathiri mtiririko wa maji ya Mto Nile ambayo inategemea asilimia 90 ya maji ya mto huo.

Makubaliano ya mwisho yatatiwa saini Januari 28-29, wakati ambapo mawaziri kutoka nchi tatu watakuwa wanakutana Washington.

Makubaliano ya awali ambayo yalifikiwa na Waziri wa Fedha wa Marekani na Rais wa benki ya Dunia, yanatilia maanani mahitaji ya Ethiopia ya kuanza uzalishaji wa umeme mapema, lakini pia yanazungumzia hatua za kupunguza athari kwa Misri na Sudan iwapo kutakuwa na vipindi virefu vya kiangazi katika nchi hizo zilizopo kwenye mkondo wa maji ya Mto Nile.

Kufikiwa kwa makubaliano hayo kunapunguza wasiwasi uliokuwepo kati ya Ethiopia na Misri ambazo zimekuwa zikizozana tangu Ethiopia ilipoanza kujenga bwawa hilo mwaka 2011.

Ujenzi wa Bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia ukishamalizika, mradi huo unaogharimu kima cha bilioni 5 za Marekani, litakuwa ndio bwawa kubwa zaidi la uzalishaji umeme barani Afrika lenye uwezo wa 6,000MW.

Chanzo: BBC Swahili
 
Bwawa linajazwa na mto tena mto wenyewe Blue Nile kwa miaka 6 sijui 10! Hilo ni bwawa au "bahari"?
 
Sasa wamisri wanalia lia nini,mbona wao wana Aswan high Dam. After all,Maji yakifika Misri si wanayaachaga yanaenda Mediterranean sea au huwa wanayanywa yote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani waangalie asilimia ngapi ya Maji yanayopotea baharini yapelekwe kwenye hilo bwawa. Mara nyingi nchi zinakuwa na wasiwasi tu ila manufaa ya hilo bwawa ni makubwa kuliko hizo hasara. Leo Dar mvua imenyesha maji yote yameenda baharini halafu kesho tunasubiria yanayotoka Ruvu ambapo yanayokingwa kuja kutumika hata asilimia 1 hayafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtt nile na wenyewe si unategemea Victoria?
Mto nile una matawi mawili moja linaanzia ziwa victoria na jengine linaanzia Ethiopia. Hayo matawi yanakutana sudan na kuwa mto mmoja na kuelekea misri hadi bahari ya Mediteranian.

The-Nile-River-Source-The-Geopolitical-Impact-of-the-Nile-Stratfor-Global.png
 
Hiyo ni Blue Nile river, siyo rive Nile. Blue Nile inachangia 80% ya maji yote ya mtu Nile.
Ila kwa mujibu wa somo lako la Historia yako Kizalendo uliyoisoma ni kwamba ziwa Victoria ndiyo kila kitu kwa mto Nile.
Haya sawa
 
Mbona hatujashirikishwa na sisi tuna umuhimu, tutakata ohooo! kumbe hata maji wangepata huku kwetu na wakaishi vyema wanaikaba maskini Ethiopia ya watu bureee!

Majukuu ya kaburu bana ni mikaburu tu, uchoyo uchoyo tuuu! maji yapotea baharini bure , watu weusi wanataka kutumia kuondoa umaskini hamtaki heee!

Nadhani hawa tusiongee sana, wapewe kichapo cha bure akili ziwakae sawa kwanza!

Baada ya hapo ndo wakae wazungumze, mna wabembeleza mno! wakijidai kushadadia vita ndo tunakata kabisaaa mwelekeo wa maji km hawaja jamba jamba.silaha tosha!
 
Mbona hatujashirikishwa na sisi tuna umuhimu, tutakata ohooo! kumbe hata maji wangepata huku kwetu na wakaishi vyema wanaikaba maskini Ethiopia ya watu bureee!

Majukuu ya kaburu bana ni mikaburu tu, uchoyo uchoyo tuuu! maji yapotea baharini bure , watu weusi wanataka kutumia kuondoa umaskini hamtaki heee!

Nadhani hawa tusiongee sana, wapewe kichapo cha bure akili ziwakae sawa kwanza!

Baada ya hapo ndo wakae wazungumze, mna wabembeleza mno! wakijidai kushadadia vita ndo tunakata kabisaaa mwelekeo wa maji km hawaja jamba jamba.silaha tosha!
Issue hii hatuhusiki Mkuu. Mto Nile una tributaries kuu mbili. Ya kwanza ni White Nile inayoaminika kuanzia DR Congo/Burundi/Rwanda/Tanzania/L. Victoria/Uganda/S. Sudan/Sudan (meets Blue Nile at Khartoum). Na ya pili ni Blue Nile inayoanzia L. Tana Ethiopia/Sudan (meets White Nile at Khartoum).

Katika tributaries hizi mbili, ile ya Ethiopia (Blue Nile) inachangia 80% ya maji yanayoingia R. Nile. Ugomvi ni kwamba Ethiopia anataka "kuvuruga" flow ya maji Blue Nile and hence Nile (beyond Khartoum) kwa kujenga bwawa upande wake. Hivyo wadau wanaohusika na mgogoro huu ni wale wa Blue Nile ambao ni Ethiopia, Sudan, na Egypt.
 
Bwawa linajazwa na mto tena mto wenyewe Blue Nile kwa miaka 6 sijui 10! Hilo ni bwawa au "bahari"?
Mamaaeee misri mpaka kaingia kiwewe/ but aftr all misri ananufaika na maji hayo pia huyaacha yanaingia mediteranian sea/ pia Ana Answan dam na hakuna aliyepiga kelele
 
Back
Top Bottom