Misri yatangazwa kutokomeza Malaria kwa asilimia 100 baada ya mapambano ya zaidi ya miaka 100

Misri yatangazwa kutokomeza Malaria kwa asilimia 100 baada ya mapambano ya zaidi ya miaka 100

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rasmi nchi ya Misri imepatiwa cheti cha kutokuwepo kwa malaria katika nchi hiyo na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo shirika hilo liliita mafanikio haya ya kihistoria.

Soma pia:
"Malaria ni ugonjwa wa zamani sana kama Wamisri wenyewe" alisema mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika taarifa yake ya siku ya Jumapili. "Cheti hiki cha Misri kama nchi isiyo na malaria ni cha kihistoria kweli, na ni ushahidi wa namna watu walivyojitolea katika kutokomeza ugonjwa huu wa kale."

Kwa kiwango cha kimataifa, nchi 44 zimepatiwa cheti cha kutokomezwa kwa Malaria.

Cheti hicho cha kutokomeza Malaria hutolewa na WHO kigezo kikiwa kuokomezwa kwa mambukizi yoyote kote kwa angalau miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Source: Aljazeera
 
Malaria, ugonjwa hatari unaoweza kuua binadamu unaosababishwa na kimelea anayeitwa plasmodium anayeenezwa na mbu jike aina ya anofelesi, umetokomezwa kabisa nchini Misri, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza Jumapili hii, Oktoba 20.

"Malaria ni ugonjwa wa zamani kama ustaarabu wa Misri yenyewe, lakini ugonjwa uliowapata mafarao sasa ni wa historia yake na sio mustakabali wake," mkuu wa WHO Tedros Adhanom amesema katika taarifa.
Je hii bongo tutafanikiwa?

Tanzania inawezekana kuutokomeza pia. Projects za Malaria ni nyingi, mikakati ni mingi. Tujifunze hapo tujue tunafeli wapi??
images (1).jpeg
 
Vitu kama hivi ndio ambavyo huaga sijui kwanini viongozi wetu hawawezi kuviiga? Sasa hvi tunae boss mkubwa wa WHO ambaye amewahi kua naibu waziri wetu wa afya, hawezi kufanya mipango na sisi tukawa na zero malaria into our country? Tuachane na kusifiana vyeti sijui exposure, sijui nani katembea zaidi duniani kuliko nani? Tuletewe matokeo, tuyaone matokeo kupitia hivo vyeti vya shule, tuone viongozi wetu wakiiga vitu vizuri walivo viona huko walikokwenda kutembea, hivo yaani
 
Sasa rasmi Misri itakuwa ikija Afrika ili kufanya utalii wa kuwatazama mbu. Sijui umenielewa?
 
Wanajotahidi sana, na wakifanikiwa tu...Wabantu watawapelekea
 
Sasa watu wamepambana 100yrs kuifanya nchi yao kuwa free from Malaria na kuifanya sehemu salama, sisi huku tunachekacheka tu na kuwa machawa wa wanasiasa.
Inabidi tubadilike sana. Hii nchi sijui tutaiendesha kwa uchawa mpaka lini
 
Vitu kama hivi ndio ambavyo huaga sijui kwanini viongozi wetu hawawezi kuviiga? Sasa hvi tunae boss mkubwa wa WHO ambaye amewahi kua naibu waziri wetu wa afya, hawezi kufanya mipango na sisi tukawa na zero malaria into our country? Tuachane na kusifiana vyeti sijui exposure, sijui nani katembea zaidi duniani kuliko nani? Tuletewe matokeo, tuyaone matokeo kupitia hivo vyeti vya shule, tuone viongozi wetu wakiiga vitu vizuri walivo viona huko walikokwenda kutembea, hivo yaani
Hapo ni hela imetumika,ukiambiwa uchange buku kila wiki la kutokomeza malaria utakubali,au utalia kama too?..jakaya alijenga kiwanda cha dawa kutokomeza mbu pale kibaha Ili kila halmashauri ipulizie halmashauri yake,wazungu wakaingilia Kati Ili waendelee kutuuzia dawa za malaria
 
Jana tu kuna mwanangu alikua anabwia mseto.

Gonjwa la ajabu na aibu kabisa hili, kuna malaria na kipindupindu naonaga ni magonjwa ya hovyo sana kama nchi kua nayo na ya aibu mno.
 
Back
Top Bottom