Shindano la Miss World 2019 limefanyika kwa mara ya 69 hapo jana tarehe 14 Desemba katika Ukumbi wa ExCeL London Jijini London, Uingereza ambapo mrembo Toni-Ann Singh wa Jamaica ametwaa taji.
Hii ni mara ya nne kwa Jamaica kupata taji hili na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1993. Kabla ya hapo ilichukua taji hilo mwaka 1963 na 1976.
Singh ana umri wa miaka 23 na ni mhitimu Chuo Kikuu cha Florida alipokuwa akisoma masomo ya saikolojia na wanawake.
Mshindi wa pili alikuwa mrembo kutoka Ufaransa huku wa tatu akitokea India. Tanzania iliwakilishwa na Sylivia Sebastian.
Waandaaji wa miss Tanzania inabidi waji re-evaluate. Angalia watu wanaopelekwa na nchi za wenzetu. They are eloquent educated and have university degrees. Huku kwetu wanachukua watoto wa miaka 18 hata uwezo wa kuunda sentesi ya kiingereza hawana. Wapo busy na outer beauty hawajiulizi wana nini kichwani