Ahsante X-PASTER kwa kuurudisha uzuri nyumbani, maana kuna wakati nilifikiri wote tushalewa mvinyo wa uzungu na kusujudia kila kitu cheupe, hata wale tuliowasema "wazuri weusi" wakawa shurti wawe wamepigwa msasa wa uzungu na kuvikwa u Mariah Carey, Halle Berry na Beyonce.
Kumbe tuna vyetu pure vipusa. Halafu umkute huyu mzuri nje na ndani, ana tabia za kiafrika zenyewe, utafurahi na roho yako.
Dada hayo macho na hiyo haiba ya tabasamu lisilo na tabasamu Giaconda haoni ndani.