palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,459
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) wamesema endapo mrembo wa Taifa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti Mtemvu, atabainika kudanganya umri wake kwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, atakabiliwa na kifungo cha kwenda jela kwa muda usiopungua miaka mitatu, imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Rita, Josephat Kimaro, alisema adhabu hiyo imewekwa kwa wale watakaofanya makosa ya kutoa taarifa za uongo ili waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa au kifo.
Kimaro alisema kwamba adhabu hiyo humpata mkosaji hapo hapo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa taarifa zake na kulinganisha na zile alizoziwasilisha Rita ili kupatiwa cheti kipya.
"Kifungu namba 28 (3) cha sheria ya kuandikisha vizazi na vifo kimeweka adhabu kwa makosa ya kutoa habari za uongo na adhabu hiyo hutolewa hapo kwa hapo," alisema Kimaro.
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (sura ya 108) toleo la mwaka 2002, ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili, na pia kosa la jinai kughushi.
Alisema kwa sasa suala la Sitti limepelekwa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo (Philip Saliboko) na mara baada ya kukamilika taarifa zake zitatolewa hadharani ili jamii ifahamu ukweli.
"Huo mkanganyiko tumeshaupokea na tunaufanyia kazi, tutafanya kazi hii kwa kuzingatia na kufuata sheria na miongozo," Kimaro alisema.
"Rita imebaini kuwapo na udanganyifu wa aina hiyo ambao unafanywa na waombaji kwa kutuma maombi mapya baada ya kutakiwa kupeleka vyeti ili wapate ajira, kujiunga na vyuo au kusafiri nje ya nchi.
Alisema pia wengine wamebainika kuomba vyeti vipya wakiwa na nia ya kubadili majina na kuyaacha yale ya awali waliyokuwa wanayatumia kwa sababu binafsi wanazozifahamu.
Alisema kwamba watachunguza kama mrembo huyo alifuata taratibu zinazostahili za kuomba cheti kipya ikiwapo kuwasilisha taarifa ya kupoteza cheti hicho inayotolewa katika kituo cha polisi.
Mapema Jumanne wiki hii, Sitti, alishindwa kusema ni kituo kipi alitoa taarifa baada ya kupoteza cheti chake cha kuzaliwa cha zamani huku pia akishindwa kukubali au kuikana hati yake ya kusafiria ambayo inayoonesha amezaliwa Mei 31, 1989 na ilitolewa Februari 15, 2007 na muda wake wa kutumika mwsiho ukiwa ni Februari 14, 2017.
Hati hiyo ina namba AB 202696 wakati cheti kipya cha kuzaliwa kilichotolewa Septemba 9, mwaka huu kinachoonesha amezaliwa Mei 31, 1991 ni namba 1000580309.
Katika cheti hicho kipya kinaonyesha kuwa baba wa Sitti ni Abbas Mtemvu Zuberi (Mbunge- Temeke) wakati mama yake ni Mariam Nassor Juma (Diwani- Temeke) jijini.
Hata hivyo, NIPASHE lilipotinga Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kutaka kujiridhisha kuhusu utata wa umri wa Sitti, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Ilovia alisema wameshapokea maswali mengi kutoka kwa waandishi, hivyo kwa sasa wanafanya uchunguzi na utakapokamilika wataitisha mkutano na wanahabari ili kuujulisha umma ukweli halisi.
Sitti aliibuka kidedea katika shindano la urembo la taifa lililofanyika usiku wa Jumamosi ya Oktoba 11 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini na kuwashinda washiriki wenzake 29 waliokuwa wanawania taji hilo.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
>>>>HAPA CHINI NI TAARIFA KUTOKA IDARA YA UHAMIAJI MAREKANI>>>>>