Miss Tanzania 2018: Mimi ni Mlokole, nampenda Yesu Kristo

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na EATV. Kasema kila shindano alikuwa anashinda, na siri ya Ushindi ni Maomba ya Baba mchungaji wake wa Kiroho.

"Mimi naishi magotini mwa bwana".

Baada ya mashindano ya Miss Tanzania kukamilika na Queen Elizabeth Makune kuibuka mshindi wa taji hilo kwa mwaka 2018, wazazi wake wameibuka na kusema kwamba mtoto wao ameokoka na anamtumikia Mungu.

Akiongea kupitia eNewz mama wa mrembo huyo amesema kwamba mtoto wake amekuwa akipenda sana kuvaa ‘crown’ tangu akiwa mdogo, kwani hata wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alikuwa anapenda kununuliwa keki ambayo ina ‘crown’ juu.

Hata hivyo mama Queen Elizabeth ameendelea kusema kwamba “Queen ni mtoto wa kanisa hata kabla hajawa ‘star’, alikuwa anakaa mlangoni kanisani kwa ajili ya kupokea na hata alipokuwa anachukua mataji mbalimbali kabla la Miss Tanzania alikuwa akienda kanisani na kuomba aombewe ili kuweza kufika mbali zaidi”

Kwa upande wake, Miss Tanzania Queen Elizabeth Makune amesema anajisikia furaha kupata nafasi hiyo na kudai atahakikisha kupambana na kuipigania Tanzania zaidi ya Miss Tanzania 2016/2018 Diana alivyokuwa
 
Tumpeni muda tu, tusiwe na haraka. Maana ukiwa miss unakutana na vimbwanga, utaruka vihunzi kinoma.

Utahongwa hela, utakataa. Watapanda dau uhongwe gari, utakataa. Dau litazidi uhongwe nyumba, ndo utakapo jitathmini uendelee na msimamo wako au uvue chupi.

Kama hataishia kuwa kama kina Wema.
 
Basi wadada wataokoka wote ili mwaka ujao wawe miss Tanzania.....tigo pesa ni zaidi ya pesa
 
Hivi yule Hashim Lundenga bado yupo au amestaafu?

Nasikia amebakia kuwa mdau tu!
 
ok baada ya muda hatutarajii kusika huyu Makune anakunwa!!!! kama hawa wengine akina sepenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…