Miss Tanzania Diana Flave alia hajapewa zawadi wala hakuna maandalizi ya Miss world

mchepuko

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,192
Reaction score
1,415

Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World’, ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza hali ambayo amedai inaweza kumfanya ashindwe kuiwakilista Tanzania katika mashindano hayo.

Mrembo huyo amedai bado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.

“Hata zawadi zangu zilizo haidiwa sijapewa, kwahiyo inakuwa ngumu kwangu kujiandaa na mashindano ya miss dunia,” Diana alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Siku ishirini zilizobaki ni ndogo natakiwa kuandaa documentary ya historia ya kimasai Arusha. Sina kitu chochote chakufanyia natakiwa nilipe hiyo, natakiwa nilipe team support kwa sababu natakiwa kwenda kuonyesha Tanzania yangu, natakiwa kuonyesha beauty of purpose,”

Aliongeza, “Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve”

Kwa upande wa afisa uhusiano wa kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico amesema shughuli za maandalizi ya miss huyo zinafanywa na Kamati ya Miss Tanzania.

“Hayo mambo yanashughulikuwa na Kamati ya Miss Tanzania. Yaani ameshaanza kuongea na vyombo vya habari? Mimi sina mamlaka ya kulijibu hilo la zawadi lakini nachojua maandalizi yake yanafanyika na kamati,” alisema Rico.
 
hehehe Hoyce Temu mpeni mtoto zawadi yakee
 
Apewe bhana akaiwakilishe Taifa, she is beautiful
 
Hii miss Tanzania ishakuwa janga ni heri ifutwe maana ishapoteza mvuto kwa kweli
Na mabinti wanaoshiriki hawaeleweki full kuzeeka
 
Mkome,mlifikiri maisha ni kuonesha vipapatio na vipaja visivyo na nyama wakati mwingine kugongwa gongwa.Kama hajapata zawadi si atulie tuu kwani ni lazima kwenda miss world,walioenda wote toka enzi za mama yake Le Mutuzz walililetea nini taifa?
 
Acheni mamboa ya kucheka cheka eti ndo mnatafuta maisha,mtaishia kuwa ama wauza migegedo au mapunda wabeba sembe
 
lundenga inabidi atimuliwe miss tanzania...

uncle magu lazima afutilie mbali huu ujinga
 
Mkome,mlifikiri maisha ni kuonesha vipapatio na vipaja visivyo na nyama wakati mwingine kugongwa gongwa.Kama hajapata zawadi si atulie tuu kwani ni lazima kwenda miss world,walioenda wote toka enzi za mama yake Le Mutuzz walililetea nini taifa?
Mama ake LEMUTUZ?
 
hahaa mi staki
 
Mimi nashindwa hata kuelewa huyu HASHIMU LUNDENGA anafanya nini mpaka sasa kwenye MISS TANZANIA..

Nape Nnauye tunaomba uisambaratishe hii kamati iliyozeeka ya Miss Tanzania jamani,yaani kweli tunafelishwa na kina Lundenga na wenzie jamani kwa maslahi yao binafsi?!

Wapeni wakina JOKATE na K-LYNN hii mikoba muone mabadiliko,linakera sana hili swala.
 
Miss Tanzania inapaswa ifutwe na kama inaendelea isitumie jina Tanzania maana ni aibu
 
KAMA HAMTAKI AKAIWAKILISHE HIYO NCHI YENU,BASI MPENI ZAWADI ZAKE ANAZOSTAHILI.
 
Mkome,mlifikiri maisha ni kuonesha vipapatio na vipaja visivyo na nyama wakati mwingine kugongwa gongwa.Kama hajapata zawadi si atulie tuu kwani ni lazima kwenda miss world,walioenda wote toka enzi za mama yake Le Mutuzz walililetea nini taifa?
Nimechekaa eti toka Enzi ya mamaake Le Mutuz watu mna maneno!
 
Kwani huyu Lundenga ndio SI unit ya hayo mashindano wadau?nimemsikia huyu jamaa tokea sijaanza kuota ndevu,sasa ndevu zimeota mpaka zinaanza kuota mvi bado nasikia Lundenga,hii naona ipo Tanzania pekee,abakie sasa kuwa mshauri tu awapishe na wengine wasonge mbele na hiyo kazi.
 
Mkome,mlifikiri maisha ni kuonesha vipapatio na vipaja visivyo na nyama wakati mwingine kugongwa gongwa.Kama hajapata zawadi si atulie tuu kwani ni lazima kwenda miss world,walioenda wote toka enzi za mama yake Le Mutuzz walililetea nini taifa?
Punguza hasira miss kanda ya nyonyo.
Unatokwa povu bz uliliwa bure halafu wakapewa watu wenye vigezo vyao. Pole, jikande tuu kitapoa.
 
Mkome,mlifikiri maisha ni kuonesha vipapatio na vipaja visivyo na nyama wakati mwingine kugongwa gongwa.Kama hajapata zawadi si atulie tuu kwani ni lazima kwenda miss world,walioenda wote toka enzi za mama yake Le Mutuzz walililetea nini taifa?
Eeeeehhhh, kumbe ndo maana King of all social media tasnia ya wabebez ni inborn character........??? No wonder at his age alikesha Fiesta na wabebez wakareee hadi saa 12 asbh...................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…