Miss Tanzania namba 2 (Lilian Kamazima) ''ana tatizo la uraia''

Wanajamvi tumekuwa na msuguano kuhusu Urai wa Jenerali KAMAZIAMA; kuhusu uraia wake na hili linaturudisha kule kule kuwa asili ya miss Tanzania ni Mnyarwanda.

Uchunguzi uanze upya
Mkuu R.B, hili haliwezi kuwepo, Generali Anatole Pascal Kamazima, ametumikia jeshi letu maisha yake yote!, kama issue ni uasili, hiyo sio issue kabisa kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya uraia, watu wote walikuwa ndani ya ardhi ya Tanganyika kuanzia saa 6:00 usiku wa Dec, 1961, watahesabika ni raia halali wa Tanganyika huru, regarless asili zao!.

Tukianza na chimba chimba za nani alitoka wapi na asili yake ni wapi, mtakuja kukuta Watanzania Halisi ni Wasukuma na Wagogo na makabila mengine machache!.

Tukianzia na Mkombozi wetu, inasemekani huyu baba yake ambaye ni Chifu, alitoka Rwanda, uchifu wakati ule ukitolewa kwa mwenye ng'ombe wengi!, bila kuuliza alikotoka!.

Tukija kwa yule wa Zanzibar, alitokea Malawi, na wanae wote wamesomea kwa babu yao tangu shule ya msingi!.

Hata "Che Nka!", kwanza hilo jina ni la kikeni!, na alikuja nchini akiwa na miaka 6 huku akitembea mwenyewe kwa miguu yake miwili!.

Wangoni wanajulikana walikotoka, wakiongozwa na Zongendamba!. Wamasai na Wachaga wanajulikana walikotoka!. Wahaya na Wahangaza wanajulikana fika ni sehemu ya dola ya Bunyoro!. Musoma karibu wote wametokea kule!. Kigoma karibu wote wametokea kule!.

Wanyasa ni jina tuu, kiukweli ni Wamalawi!. Wamakonde hakuna siri wote wanatoka "nchumbiji!.

Tusifikishane huko tukaanza kunyoosheane vidole kila mmoja arudi kwenye asili yake!.

Pasco
 
Ni muhayaaa kwa upande wa baba na mamake ni mchagaaa katoto ka juz tunakaona kanaruka rege mitaa ya stand ndogoo## Anajulikana kama mzee mwana mwanaa
 
Ni mtanzania amezaliwa tanzania amesoma chuo cha uhasibu arusha na alikua mshiriki wa miss chuo mwaka huu....hayo mafekero yenu kama mmetumwa peleken kwa wake zenu na waume zenu..usikute umekaa hapo wewe unaongea kumbe ni mkongo...mxxiiiwww we are sick and tired!!

Ova
 
Hili shindano limekosa hadhi kabisa.ubabaishaji umekuwa mwingi mno..
 
Apewe wa 3 au mchuano urudiwe
 
Kweli inatupasa kufuatilia mambo ya msingi na yakujenga nchi.si mambo ya misw tz kila mda
 
Wasitutoe kwenye mada kuu: siti rudisha taji, hizi njama za baba ake siti anazotumia kupata ubunge, achafue wapinzani wake yeye apete, SITTI rudisha taji bana kwani sh ngapi?
 
Hahahahaha! Wa 3 atakua alikua kidume akabadili jinsia! Sitashangaa!
Embu jadilini mambo mengine sasa, huo u miss umempa faida gani mtu yeyote wa pembeni zaidi ya huyo miss na ndugu zake!?

Tunashupalia mambo yasio na umuhimu sana kwetu kwa kweli.
Don't be ridiculous.

Wewe unajadili halafu wengine unataka wajadili mambo mengine muhimu, na hizo comment zako hapo kuhusu mshindi wa tatu ni nini hizo, ibara za rasimu?
 
Wasitutoe kwenye mada kuu: siti rudisha taji, hizi njama za baba ake siti anazotumia kupata ubunge, achafue wapinzani wake yeye apete, SITTI rudisha taji bana kwani sh ngapi?

Wanataka kutoa watu kwenye mada kuu.Hela hajarudisha pamoja na mataji ya Temeke na kitongoji
 
Huyu lilian ni MNYARWANDA original.. Ndugu yake na Kagame
 
Rwanda ina mamiss wawili sasa. Miss Rwanda na Miss Tanzania.
 
mbona sijawahi kusikia Miss kutoka Zanzibar?au si Tanzania ile?
 
Ndio maana mashindano ya mwaka huu yalishaanza mizengwe tangu hatua ya maandalizi hadi kufikia hatua ya kupelekana mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…