Miss world yafuta vazi la ufukweni

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,227


Waandaaji wa mashindano ya urembo ya dunia maarufu kama Miss World wamefuta sehemu ya shindano hilo inayohusisha warembo wakiwa wamevalia nguo za kuogelea maarufu kama vazi la ufukweni au Beach Wear.

Mkurugenzi wa mashindano haya Chris Wilmer amesema kuwa sababu ya kfuutwa kwa kipengele cha mashindano ya cha nguo ya kuogelea ni kushindwa kuendana na vipengele vingine vya mashindano haya .

Mkurugenzi huyo amesema kuwa mashindano haya pamoja na kuwa mashindano ya urembo lakini hayahusishi urembo pekee bali urembo na sababu maalum na hakukuwa na sababu yoyote maalum ya kujumuisha kipengele cha nguo za kuogelea.


Miss World imeamua kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mshindi wa Miss World anapaswa kuwa balozi na msemaji wa jamii ya watu sio malkia wa urembo pekee .

Maadili na kile anachowakilisha mshindi wa Miss World ndio kinachotazamwa kwa mshindi hivyo kwa sababu hiyo Miss World haitakuwa na kipengele cha shindano la nguo ya kuogelea .

Kipengele hiki kimekuwepo tangu mwaka 2001 wakati kilipopewa jina Beach Fashion huku kikifanywa kama kipengele binafsi ndani ya shindano hilo.

Kwa Hisani ya MillardAyo.com
 
Nachukulia hii hatua kama hatua ya muhimu sana kulipatia hili shindano hadhi inayostahili

Miss world ni shindano linalokutanisha watu wenye tamaduni na maadili tofauti

Kuna mataifa mengine ambayo ile tu mtu kuonekana mtupu ni dhambi

Kudos kwa miss world
 
Tunakoelekea ni kama sasa wazungu wanajutia kwa waliyoyafanya/wanayoyafanya....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…