A
Anonymous
Guest
Hivi suala la kujengea Wanafunzi vyoo ni la wakina nani? Maana kuna shule moja Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera inaitwa "Mugana A" kwakweli hali sio nzuri.
Vijana hawana vyoo salama kabisa, sasa sijajua wahusika hawapo, make hili tatizo lina muda mrefu na hali inazidi kuwa mbaya kwani pamoja na kuwa vyoo ni vichache bado vimechakaa, havina miundombinu ya maji; jambo ambalo ni hatarishi kwa vijana wetu.
Naombeni wahusika muwafikirie Watoto hawa na mvae uhusika kama nanyi watoto wenu wangesomea mazingira hayo.