KERO Missenyi, Kagera: Watoto hawana vyoo salama Shule ya Msingi Mugana 'A'

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Jamani,

Hivi suala la kujengea Wanafunzi vyoo ni la wakina nani? Maana kuna shule moja Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera inaitwa "Mugana A" kwakweli hali sio nzuri.

Vijana hawana vyoo salama kabisa, sasa sijajua wahusika hawapo, make hili tatizo lina muda mrefu na hali inazidi kuwa mbaya kwani pamoja na kuwa vyoo ni vichache bado vimechakaa, havina miundombinu ya maji; jambo ambalo ni hatarishi kwa vijana wetu.

Naombeni wahusika muwafikirie Watoto hawa na mvae uhusika kama nanyi watoto wenu wangesomea mazingira hayo.




kielelezo:hizo ni baadhi ya picha za vyoo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…