Mission failed kwa GSM

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
1,712
Reaction score
2,577
Mpango wa GSM kuwa mdhamini mwenza unaanza kukutana na changamoto.

Nadiriki kusema kwamba mapungufu ya mkataba yasingejadiliwa kama:-
1) Mbele ya media kusengekua na sura za uyanga wakati wa utiaji saini wa mkataba.

2) Post tata za Manara mitandaoni kuhusu kuwamiliki Simba kupitia mkataba wa GSM kwenye udhamini mwenza ligi kuu ya NBC.

3) TFF na Body ya ligi kutumia nguvu kubwa kuliko busara kwenye swala la Simba kuvaa nembo za GSM.

GSM wajipange upya wanalolitaka litatimia kwa busara.
 
Mkataba wa GSM na tff upo pale pale,busara imetumika ili tu kesho msikimbie,baada ya hapo ndio mtajua hamjui,hamna sapoti ya timu hata 1 kwenye ligi yenye timu 16,tunawasubiri mkagomee mabango mkicheza na kmc ili tuanze kuwanyoosha kikanuni
 
mazuzu. Utopwinyo. 😂😂😂😂😂
 
Mkataba wa GSM na tff upo pale pale,busara imetumika ili tu kesho msikimbie,baada ya hapo ndio mtajua hamjui,hamna sapoti ya timu hata 2 kwenye ligi yenye timu 16,tunawasubiri mkagomee mabango mkicheza na kmc ili tuanze kuwanyoosha kikanuni
Hatuhitaji sapoti katika kusimamia kanuni zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mpango wa gsm kuwa mdhamini mwenza unaanza kukutana na changamoto.
Nadiriki kusema kwamba mapungufu ya mkataba yasingejadiliwa kama...
GSM hakua na mpango wa kudhamini ligi ila alifatwa.
 
Haiwezi kua imefeli mpaka sasa tayari amewin katika tumemtangaza zaidi kuliko simba wange kubali kuivaa
 
Hatuhitaji sapoti katika kusimamia kanuni zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Wanaosimamia kanuni ya mpira wetu ndio washasema,wewe upinge nani,busara imetumika ili kesho mlete timu lenu tulibutue goli za kutosha,baada ya kesho ugomee tena match zijazo ili ukutane na kitu kizito cha utosi,GSM bado mdhamini mwenza wa ligi yetu na kwa umbumbu wenu mnadhani mtashinda hii challenge while ligi ina ina timu 16 then huu umbumbu mpo peke yenu,hamna timu yoyote inayowaunga mkono

 
Mkataba wa GSM na tff upo pale pale,busara imetumika ili tu kesho msikimbie,baada ya hapo ndio mtajua hamjui,hamna sapoti ya timu hata 1 kwenye ligi yenye timu 16,tunawasubiri mkagomee mabango mkicheza na kmc ili tuanze kuwanyoosha kikanuni
Sasa hapo ndo wataharibu... Hv watawalazimishaje Simba au club ingine kuvaa na kuweka mabango ikiwa mechi ya kwanza iliopaswa kuwekwa yalitolewa tena bora wangezuga wasiweke kabisa ila wameweka kisha wakayatoa unapataje moral authority ya kulazimisha tena.. Ukiulizwa kwa nini ulitoa kama hakukuwa na makando makando utasema nini? Kuwa Busara ilitumika...

Mpira wa Nchi hii unaharibiwa na Busara kutumika.. Yanga waligomea rangi za NBC ikatumika Busara... Na leo tena ya Simba na GSM so TFF wakisema Busara itumike ndo wameharibu zaidi

Bora TFF wajiangalie upya...
 
Kesho kuna match nyingine,na timu zitavaa nembo ya gsm na mabango yatakuwepo,tunawasubiri kolo wakienda kucheza na kmc kama mabango yatatolewa na wasipovaa nembo faini,kesho imetumika busara tu ili wasikimbie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…