Mission to Saturn (Cassini–Huygens)

Mission to Saturn (Cassini–Huygens)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Mission to Saturn
1580124411624.png

Mwaka 1997 Nchi za Mrekani, Itali na umoja wa ulaya zilianzisha mission ya kwenda kufanya utafiti kwenye sayari ya Zohali (Saturn). Misheni hiyo ilijulikana kwa jina la Cassini.
Misheni hiyo ilichukua miaka 19 na siku 335. Yaani kwamba siku ya 335 ya mwaka 20 ndipo chombo hicho kiliigia katika anga la sayari ya Zohali. Kulingana na anga hilo kuwa na mkusanyiko mkubwa wa gesi. Kiliweza kuteketea na kuwa sehemu ya sayari hiyo.


Jinsi ya safari ilivyokuwa
1580125017335.png

Safari ya kwenda kwenye anga za mbali zinatakiwa kwenda kwa timing.

Chombo kilindoka duniani mwaka 1997. Ifuatayo ni Time frame ya chombo hicho:

1. 15 October 1997: Kilindoka duniani launched at 08:43 UTC.

2. 26 April 1998 06:52 PDT: iliingia katika sayari ya venus. Yaani liingia ndani kidogo kuelekea kwenye jua. Wanaita Gravity-assisted flyby of Venus at 284 km. Ilipata Booster ya speed na kuwa na speed ya 7km/s


3. 18 August 1999 03:28 UTC kiliigia katika orbit ya dunia na kupata booster tena

4. 30 December 2000 10:05 UTC kiliingia kwenye sayari ya Jupiter. Yaani miaka mitatu baada ya kuanza safari.
1 July 2004 – The Saturn Orbit Insertion burn was successfully executed
1580126998643.png


Naomba tuendelee kidogo. Weka comment yako....
Nitaendelea kuhusu details za mission hiyo.
 
Natafuta uhalisia hapa,
Ila endelea kwanza kabla sijakomenti
 
Hu Uzi hautanoga bila Kiranga au da Vinci kiranga namkubali Sana nasubiri siku afumue uzi
 
Hu Uzi hautanoga bila Kiranga au da Vinci kiranga namkubali Sana nasubiri siku afumue uzi
Shukurani sana mkuu, huwa nafurahi sana kuona vitu adimu vinawekwa katika Kiswahili.

Natamani nilivyokuwa nakua kungekuwa na mitandao kama hii.

Watoto wa siku hizi wanapata raha sana kupata habari hizi kwa urahisi, enzi zetu lazima mtu uzunguke British Council, USIS Peugeot House na Mkataba Kuu ya Taifa kupata vitabu vizuri vyenye kuelezea habari hizi.
 
Za asubuhi tena ndugu zangu. Nitaendela kuelezea hii misheni ya kwenda kwenye sayari ya Zohali. Kuna wengine watapinga kwamba hii misheni ni ujanja ujanja wa wenzetu waliotutangulia kiteknolojia, wengine watakubaliana na suala la misheni hii, lakini wengine watabaki katikati kusubiri ujuzi wao na utafiti wao binafsi.

Kwa watu wasomi na wenye upeo mpana wa kutafiti mambo huwa wanakuwa katikati na kusubir wafanye utafiti wao ili kuleta utafiti mpya.

Sasa basi kwakuwa hakuna utafiti mwingine uliofaywa na kufanya misheni ya kwenda kwenye sayari hii, basi itabidi tufuatilie misheni hii ya wenzetu ili aidha kujifunza au kujua namna walivyofanya ilikwamba na sisi tuweze kuanzia pale.

Hata hivyo kwakuwa tunakubaliana kwamba zipo sayari kama dunia zinazunguka jua, basi itabidi tufikirie namna ipi tuweze kuzifikia sayari zingine. Kama wataalamu wa kale (wanajimu)akina Galileo Galilei waliweza kutumia darubini na kuona sayari mbalimbali, sisi kizazi cha sasa tuna wajibu wa kwenda mbali zaidi ya pale.

Sasa basi nitakuwa na mfululizo wa vipindi na maandiko mbalimbali ya kuhusu uchunguzi na misheni za kwenda kwenye anga za juu mbali.

MISHENI CASSINI
Kama nilivyotoa utangulizi hapo awali, misheni hii ilikuwa na lengo la kwenda kwenye sayari hii ya maajabu na kufanya uchunguzi.

Safari hii ilitumia miongo miwili, na ilikuwa imegawanyika katika misheni tatu:-

  • Primary mission
  • Cassini Equinox Mission
  • Cassini Solstice Mission
Primary Mission
Lengo kuu la mishieni hii ni kupata kuijua sayari hii, mazingira yake na miezi(setelite) zinazoizunguka.

Katika safari yake ya kutoka duniani chombo hicho kilifanikiwa kupiga picha kadhaa za sayari ya Sumbula (Jupiter).

1580200215105.png

Hii picha ilipigwa na chombo hicho December 29, 2000 kutoka umbali wa takilibani kilomita milioni kumi (10,000,000km)

Ngoja kwa sasa nipumue kidogo kisha tutaendeleza mjadala huu mkubwa wa kisomi.
 
Primary Mission
Sayari hii ya Zohali inakadiliwa kuwa na miezi 82, kati ya hiyo miezi 53 imethibitishwa na kupatiwa majina lakini miezi mingine 29 bado wachunguzi wapo katika uchunguzi wao.

Moja ya misheni hii ilikuwa ni kwenda kufanyia uchunguzi mwezi mkubwa(Titan) uliopo katika sayari hii. Mwezi huo ulivuta hisia za wanajimu wengi walipokuwa wakitumia darubini zao. Mwezi huo ulisemekana kuwa na hali ya hewa kama ya hapa duniani. Yaani mwezi huo ulikuwa na mvua, mawingu na hewa ya nitrojeni.

Wajilogia mwaka huu wamekamilisha kutengeneza ramani ya mwezi huo, kama ifuatavyo hapa chini:-
1580205015066.png

Ngoja nibaki katika misheni hii.
Ngoja tuongelea Huygens kwa sababu sina maelezo mwazuri ya kiswahili ngoja nichanganye na lugha ya kingereza:

What was Huygens?
ESA's Huygen's probe was designed to study the smog-like atmosphere of Saturn's largest moon Titan as it parachuted to the surface. It also carried cameras to photograph the moon's surface. Huygen's traveled to Saturn aboard NASA's Cassini orbiter.

Baada ya kuelewa maana yake, ngoja sasa tuangalie ni vifaa vipi vilikuwa vimebebwa na chombo hiki:-

1. Atmospheric Structure Instrument (HASI)
2. Gas Chromatograph Neutral Mass Spectrometer (GC/MS)
3. Aerosol Collector and Pyrolyzer (ACP)
4. Descent Imager/Spectral Radiometer (DISR)
5. Surface Science Package (SSP)
6. Doppler Wind Experiment (DWE)

Picha hapa chini ni ya Huygen kikiwa katika uso wa Titan
1580205831979.png



Hii hapa chini ni picha iliyotumwa na kifaa hicho wakati kikielekea kwenye uso wa Titan. Picha hii ilitumwa January 14, 2005.
1580205899993.png


Hapa chini ni mwonekano wa mwezi huo kwenye sayari ya Zohali

1580206209908.png


Titan Temperature Lag Maps & Animation
1580206373695.png


Hii video hapa chini inaonesha namna ya kifaa kilivyokuwa kinatua katika uso wa Titan


Lengo la thread hii ni kuamsha uelewa na kutaka kujua zaidi. Naomba nitaendelea kuleta taarifa mbalimbali kwa ufupi.

Na ukitaka kupata maelezo zaidi unaweza kufuatilia na kusoma misheni hii.

Nitakuja baadae.....

 
Mkuu hivi kwa nini picha zote za hizo sayari huwa nusu either robo tatu? in short sijawahi kuona full image ya sayari.
 
Mtoa habari naona unatoa kwa kuruka ruka hukai sehemu moja ukamaliza daa..😃!!
 
Back
Top Bottom