Kwanza shikamoo daktari/Mtaalam/Mwenye kujua utatuzi wa shida hii. Habari za huko nyumbani. Natumaini hujambo. Mimi ni kijana wa miaka 32.
Nina tatizo kwamba macho yangu yana mistari mingi myekundu na jicho hili la kulia kwa juu hapa pana kama kangozi fulani kekundu. Kwa hiyo nakuomba unijulishe hili ni tatizo gani? Na unanisaidiaje katika kulitibu.
Nafikiri atakae jibu swali lako uwenda wakawa wachangiaji tofauti wenye fani na wasikuwa na fani ya Udaktari...
Kiufupi Daktari unaemuakia na kumtakia hali pamoja na kujua hali ya nyumbani atakuwa katoka:bange:
Jibu...au ushauri wangu nenda Hospitali ya macho iliyo karibu nawe alaka iwezekanavyo kama uko Dar nenda CCBRT
Tayari nimetibiwa kwa ushauri wa miwani ya kusomea (TSHS 60,000),mboga za majani kama spinachi nile na karoti. Kupunguza matumizi ya kompyuta na simu. Asanteni.