Misumari, malighafi kwa ajili ya SGR ya Tanzania vitatoka Uturuki, halafu wanaicheka Kenya

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kwa mujibu wa uchambuzi wa Zitto Kabwe, misumari, malighafi na hata makampuni ya kuchimba kokoto zitatoka kwa Waturuki. Watanzania wataishia kupokea tu basi, sasa nashangaa wale hukesha huku JF wakibeza reli ya Kenya wakati sisi tulihakikisha makampuni ya ndani yalinufaika pakubwa Local Procurement in SGR Stands at 10 Billion - Ministry of Industry, Trade and Cooperatives
-------------------------------------------------------------------

Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo, Mh.Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma, amesema kuwa, ni jambo la kushangaza kuona Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyingine nchini.

Mh.Zitto akahoji kuwa, inawezekanaje kweli hata misumari ( screws) nchi hii haiwezi kutengeneza mpaka iagizwe kutoka Uturuki na kwamba yani hata kampuni ya kuchimba kokoto itoke Uturuki,”? alihoji.

Akiendelea kuonyesha kushangazwa na jambo hilo alisema kuwa, mpaka serikali itegemee malighafi hizo kutoka nje hivi viwanda vya chuma nchini CTI, TPSF vinafanya kazi gani sasa.

“Nielezeni hili, hamuwezi kuzalisha kitu chochote kulisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR katika BOQ ya Mradi wa SGR, hamna muwezalo? Serikali iliwapa BOQ mkashindwa?” alihiji Mbunge huyo.

Akasema, ata ukiwauliza watu wa Wizara hawana majibu, wanasema Mkataba ali alifanya makubaliano Rais mwenyewe.

Aidha aliendelea kusema kuwa, inawezekanaje kuamini hili na kwamba hawezi kumuuliza rais na kwamba wao kazi yao ni kukosoa tu.

“Amekasirika, Siwezi kumwuliza mtu aliyekasirika, tena Amiri Jeshi Mkuu” alisema.

Wakati wa Mdororo wa Uchumi Asia mwaka 1997-1998 Waziri Mkuu wa Malaysia Tun Mahathir Mohammed alifanya miradi mikubwa sana ikiwemo kujenga Mji Mpya, barabara kubwa na Jengo la Petronas.

Ili kuingiza fedha kwenye uchumi na kuchochea shughuli nyengine za uchumi na kukuza mahitaji ( aggregate demand). Malaysia ikawa nchi ya kwanza kuibuka kutoka Asian Financial Crisis.

Aliongeza kuwa, sisi watawala wetu wamekwenda madarasa tofauti na kusoma vitabu tofauti vya Uchumi? Unajenga Reli kwa pesa yako ( inavyodaiwa), kwa hiyo unakusanya kodi kutoka kwa watu wako, unanunua US$, unamlipa Mkandarasi. Mkandarasi ananunua kila kitu kutoka nchini kwao Uturuki, mataruma ya Reli, Chuma, Screws na Misumari na hata mchimba kokoto Mturuki.

“Kwenye uchumi hii inaitwa leakages. Uchumi wetu unahitaji more inflows, unajengaje Reli kwa kutumia Chuma kutoka nje wakati una hazina ya chuma Ludewa?, unamwaga TZS 7 Trilioni bila kuhakikisha offsetting? Natamani kuiona hiyo BOQ ya Reli ya Kati”, akasema Mh.Zitto.

Alisema, suala hili linanisumbua sana, ni vigunu kuamini kuwa watawala waliokwenda shule na wenye uzoefu Serikalini hawakuona faida kubwa ya offsets na kwamba Baraza la Mawaziri limejaa wasomi wenye PHDs, inashangaza kuona kama ni kweli wameshindwa kuona hili.

Alimaliza kusema kuwa, fedha zetu wenyewe tunatengeneza ajira nje ya nchi huku sisi tukiwa vibarua tu na wagonga reli, Trilioni 7 zingechochea sana uchumi.akasema, kutokana na hili ni vyema watetezi wa Serikali, mnaojua kuitafsiri Serikali, lifanyieni kazi suala hili. nisaidieni.


INASHANGAZA SERIKALI KUWEKA MKATABA WA TRILIONI 7 KUJENGA RELI BILA KUSHIRIKISHA SEKTA NYINGINE- MH.ZITTO
 
Unapatia hawa watu stress mengi juu hata ujenzi haujaanza na Labda haunzishwi hivi karibuni. Hapa ni "tuta" miaka nenda miaka rudi in fact they have no definite timelines and their projects are mostly done in the present through paperwork and word of mouth but in fact they are futuristic without a realistically reliable timeline.
 
Reli ishaanza kujengwa
 
watu wapo site buda...acha porojo.
 
Hivi wewe una akili kweli?, mbona unashindwa kujenga hoja vizuri ili tuweze kuumiza vichwa wakati wa kukujibu badala yake unajenga hoja kama mwendawazimu, ujenzi wa reli toka Nairobi- Naivasha nao haupo?, kwani reli unaanza na tuta ndiyo unaweka vyuma au unaanza na vyuma ndiyo unajenga tuta?, timeframe ipi unayotafuta wakati umeambiwa kila kipande cha reli kilichokabidhiwa contractor analazimika kumaliza ndani ya miezi 36 tangu siku mkataba umesainiwa?, tangu kipande cha Dar - Morogoro kuanza kujengwa huu ni mwezi wa tano, ulitegemea tayari wawe wamelaza mataruma ya reli ndani ya kipindi hicho ambacho sehemu kubwa ni mobilization and ground cleaning?, acha kuwa kama umekunywa chang'aa, jadili kwa kutumi akili ili ujibiwe kwa kutumia akili
 
So Zitto ni reliable source? Kiluvya steel works na slippers factory Kibaha kwa ajili ya nn?
Zitto anaanza kuchanganyikiwa, ninadhani hii ni kwasababu ya Magufuli amebana kila kona upinzani unakosa agenda za kuzungumza, hicho chuma cha Liganga anachosema, hata kuanza kuzalishwa hakuna hiyo dalili, huenda reli hii ikakamilika mapema kabla hicho chuma hakijaanza kuzalshwa, ni sawa na kusema kwanini Tanzania inaagiza gesi ya kupikia toka nje wakati kuna gesi nyingi Mtwara, au kwanini Kenya na Uganda wanaagiza diesel na petrol toka nje wakati wamegundua mafuta, Zitto amekuwa mropokaji sana siku hizi
 
Tatizo ni kwamba, tunataka miradi yenye ubora wakati huo huo hatuna uwezo wa kuleta ubora huo bila kuhusisha mataifa ya nje.... Hapa ndipo huja kitu tunaita Opportunity Cost!
 
zitto alishawahi kusema tumenunua terrible teen akashindwa kuthibitisha
Zito, mwanzoni tulikuona mtu wa maana kwa kujenga hoja lakini sasa tunakuona hata jambo lenye manufaa kwa nchi unapinga ilimradi sema usikike,kama Magu amechukua agenda zenu muungeni mkono nchi isonge mbele tule migebuka ya leo leo hata huku upareni.
 
Zito, mwanzoni tulikuona mtu wa maana kwa kujenga hoja lakini sasa tunakuona hata jambo lenye manufaa kwa nchi unapinga ilimradi sema usikike,kama Magu amechukua agenda zenu muungeni mkono nchi isonge mbele tule migebuka ya leo leo hata huku upareni.
Zitto kuna vi hela vya usnitch alikuwa anapewa enzi za mkwere jk sasa hili jamaa undumilakuwili wa zito haliutambui wala hapewi commision ya kuvuruga upinzani na enzi zile zito alikuwa anatoka na hoja nzito za kitaifa kwa sababu alikuwa anapitishiwa na kwa mlango wa nyuma na CCM B" na TISS walimeguka wengine walikuwa wanafanya kazi kwa interest ya taifa na wengine walikuwa wanafanya kazi kwa interest za viongozi wa siasa.SO MSITEGEMEE ZITO KUWA HOJA ZENYE MSHIKO TENA ANAWEWESEKA PENGO LA LISSU ANAHISI ANAWEZA FIT YEYE
 
Zito, mwanzoni tulikuona mtu wa maana kwa kujenga hoja lakini sasa tunakuona hata jambo lenye manufaa kwa nchi unapinga ilimradi sema usikike,kama Magu amechukua agenda zenu muungeni mkono nchi isonge mbele tule migebuka ya leo leo hata huku upareni.

Hivi mbona huwa mnajitoa ufahamu kwa ushabiki na kugoma kumuelewa Zitto, jamaa hata huwa mnamkamata kamata badala ya kujibu hoja zake.
Hapa hajapinga mradi, ameuliza maswali ya msingi sana, na badala ya nyie kumjibu mnapambana kumjadili......
 
Hivi mbona huwa mnajitoa ufahamu kwa ushabiki na kugoma kumuelewa Zitto, jamaa hata huwa mnamkamata kamata badala ya kujibu hoja zake.
Hapa hajapinga mradi, ameuliza maswali ya msingi sana, na badala ya nyie kumjibu mnapambana kumjadili......
Ujue ndugu yangu kila zuri linachangamoto zake ,sasa hizo changamoto angeonyesha jinsi ya kuzikabili na sio kunyoshea vidole vya kukosoa.
 
Ujue ndugu yangu kila zuri linachangamoto zake ,sasa hizo changamoto angeonyesha jinsi ya kuzikabili na sio kunyoshea vidole vya kukosoa.

Hajakosoa, ameuliza maswali muhimu sana yanayohitaji majibu, amekosa majibu hata kutoka kwa wizara zote husika, sasa nyie hapa JF huwa mpo kwenye automated gear, mnajibu hoja zake kwa kumshambulia bila hata kusoma anachokiuliza.
 
Mimi nilifikiri hii ni taarifa kutoka kwa CAG kumbe inatoka kwa mtu ambaye mimi na yeye hatuna tofauti?

MK254 kwa hili ntakushusha credit bure.
 
Hivi mbona huwa mnajitoa ufahamu kwa ushabiki na kugoma kumuelewa Zitto, jamaa hata huwa mnamkamata kamata badala ya kujibu hoja zake.
Hapa hajapinga mradi, ameuliza maswali ya msingi sana, na badala ya nyie kumjibu mnapambana kumjadili......
MK254, nadhani wewe si mwanasiasa kama nilivyo mimi. Huu utaratibu wa kuamini maneno hewa ya wanasiasa jitahidi kuiepuka kulinda heshima yako.

Kama unalolosema lina uhalisia, subiri kazi ianze halafu mbivu na mbichi zitajulikana!

Huyu bwana zitto unayemshabikia aliwahi kutuhadaa hapa watanzania kuwa ana orodha yote ya viongozi wa nchi walioficha fedha zao kwenye benki za nje na akasema atataja majina yao, kiasi cha fedha walichoficha na majina ya bank hizo. Hebu waulize watanzania hapa kama aliwahi hata siku moja kuwataja hao waloficha hela. So yeye na wanasiasa wengine hawana tofauti!


Halafu unahoji kwa nini watanzania hawamwamini zito, jibu ni kwamba sio wote wasiomwamini! Wapo wanaoamini. Lakini pia haifai kuamini kila jambo analosema mwanasiasa au kutoamini kila jambo.

Hata hivyo, hakuna tofauti na wewe usivyopenda kusikia chochote kuhusu RAO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…