Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Watu wenye ulemavu wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameiomba serikali kuwawekea mazingira wezeshi ya kupiga kura kwa kuwawekea karatasi zenye maandishi ya nukta nundu yatakayowawezesha kupiga kura bila kusaidiwa na mtu yeyote.
Wamesema kutokana na zoezi la upigaji kura kuwa la siri kwa mtu anayetaka kuwachagua viongozi awapendao hivyo wakiwekewa karatasi zenye maandishi hayo yatawasaidia kuwapigia kura viongozi wanaowataka.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Usagara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Kashinje Machibya amesema hoja hiyo ni ya msingi hivyo kuahidi kulifikisha suala hilo kwenye ngazi husika.