Jamani nimejaribu kuwadadisi watoto wanayojifunza shuleni(english medium na non english medium) nimegundua kuwa bado wanafundishwa yale tuliyofundishwa zamani ambayo nadhani ni upotoshaji kwa watanzania.
mfano ukiwauliza wanafunzi haya watakupa majibu yafuatayo
Ndizi ulimwa wapi hapa duniani utajibiwa JAMAIKA
Mtu wa kwanza kuona ziwa victoria atajibu kutoka ulaya
NK
Wakati wakijibu hiyo wengine wanaishi kwa kula ndizi jumatatu hadi jumapili na kuhusu ziwa wakati wakitaja kutoka ulaya,hapo wasukuma,wahaya na wanaozunguka ziwa hilo walikuwapo tangu linakuwepo ,hivi hii mitaala si ni kupotosha wanetu?
Nadhani muuliza swali hajakosea sana na mada yake ni nzuri tu, nikiwa kama mwalimu nadhani mitaala tunayotumia ni mizuri tu tatizo ni kwamba hatufanyi changes za mara kwa mara ndo mana zinaonekana zimepitwa na wakati. Watu kama wachina zaidi ya Jiografia ya nchi yao ukimueleza kuna ramani ya africa na tunalima mazao mbalimbali hawajui kitu, so i think even though there is banana in our country but let the student know that it is not only in our country that we are growing bananas but also we can find it in other countries as well like Jamaica and so on. By that case utakuwa umesaidia kupanua jiografia yao. I think the curriculum is good even though still we need to make some revisions on it in order to be hand in hand with every day changes.Mkuu kama huna cha maana cha kuchangia hapa JF bora uanze weekend mapema ukapate moja baridi au chibuku. Unapozungumzia watoto kufundishwa ni nchi gani hulima ndizi kwa wingi duniani, wakajibu Jamaica sidhani kama wamekosea kwani ni kweli Jaaica ni moja ya nchi maarufu kwa ulimaji wa ndizi. Na isistoshe hao watoto kama ni level ya primary ni sahihi kwani unapoingia secondary mambo yanabadilika na uelewa wao unakua na hivyo kujua kwamba hata nchi nyingine zinazalisha bidhaa fulani, lakini mwanzo lazima uwepo ambao ndio huo.
Hata ukienda mataifa yaliyoendelea bado wanaanza kujifunza mambo madogo kama sehemu zingine duniani lakini kwa kuwa wameendelea kisayansi wanaboresha mitaala yao kila mwaka na kuingiza mambo ya leo taratibu. Titration inayofanyika Tanzania ni ile ile inayofanyika china tofauti inakuja tu kwamba wachina watatumia chemicals nzuri za kisasa na TZ mwananfunzi atatumi chemicals ambazo ni cheap na hivyo pengine asipate good results, nimesoma nje na nimeona mambo yalivyo.