MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,447
Baada ya kugundua kuwa mwanangu wa nursery ana masomo 7 (hajui kusoma na kuandika vizuri), wa la pili 7 na la nne ana masomo 10, nimejaribu kupitia vitabu vyao nione kama kweli vina akisi kiwango chao cha madara.
Nimeshikwa na butwaa kwa mara ya pili na nitaeleza... Hesabu za kirumi "hata kwenye hii mitaala mibovu" hufundishwa kuanzia darasa la 4. Butwaa yangu ni pale nilipokuta namba za kirumi kwenye vitabu karibu vyote vya darasa la pili kwenye exercise, namba ambazo hawajafundishwa wala hawatafundishwa mpaka wafike darasa la 4.
Mshangao mkubwa zaidi ni kukuta namba hizi zimetumika hata kwenye vitabu vya nursery.Hapo nimechoka na kusitisha zoezi langu la kuendelea kutathmini ubora wa vitabu hivi.