iliasakhamis
Member
- Jul 28, 2022
- 9
- 7
Habari wanaJF,
Napenda kushiriki nanyi kwenyw mjadala huu wa elimu "Mitaala ya elimu ni chanzo cha vijana wengi kuwa maskini"
Mitaala ya elimu ya Tanzania haimuandai kijana kuingia kwenye soko la kujiajiri ilihali serikali haina uwezo wa kuwaajiri wahitimu wote kwenye soko la ajira
Elimu yetu inawafanya vijana wengi wanapohitimu kusubiria ajira badala ya kujiajiri kutokana na haimuandai mwanafunzi kujiajiri kabla ya kuhitimu masomo yake
Mitaala yetu inapaswa kuwa ya kuwaanda vijana katika kujiajiri zaidi badala ya kusubiria ajira kutoka serikalini au kwenye makampuni binafsi
Katika hili Serikali ina wajibu wa kuboresha mitaala yake haraka ili kuokoa kizazi ambacho kimeshakua na udumavu wa akili wa ajira ,kama serikali haitafanya jukumu la kuboresha mitaala yake inazalisha wahitimu wengi wasio na ajira hvyo wadau wa elimu waweze kuishauri Serikali kuboresha mifumo na miundo ya elimu ili kuokoa vijana kuingia katika dimbwi la umasikini kwa kukosa dira na mikakati bora ya elimu ambayo haiwaandai kuingia kwenye soko la ajira mbadala badala ya zile za serikalini
Ajira mbadala ambazo zinatoa tija ya moja kwa moja kama vijana
i) Stadi za kiufundi
Katika kada hii ina fursa nyingi ambazo zinaweza kuwaanda vijana wengi katika soko la ajira mbadala na zenye tija za moja kwa moja kama
a) Ufundi magari
Katika kada hii serikali inapaswa kuiendwleza kwa kuwaandalia wanafunzi mazingira rafiki ya kujifunza ili iweze kutoa tija kwao na serikali kwa ujumla kwa kuwaanzishia karakana kubwa ambazo zitatoa ajira mbadala
b) Fundi umeme
Katika kada hii wanafunzi wanaweza kuanzishiwa makampuni mbalimbali na kutoa ajira kwa kufanya miradi binafsi na serikali katika nyanja ya umeme
c) Fani ya uhunzi
Pia vijana wanaweza kujiajiri kupita fani ya uchomeleaji na ufuaji wa vyuma
ii) Fani ya kilimo
Endapo serikali itatilia mkazo katika fani hii kwa kuwaandalia mazingira katika vyuo stadi katika fani ya kilimo vijqna waweza kupata ajira za moja kwa moja za kujiajiri katika kilimo cha kisasa ambacho kitaleta tija kwao na taifa kwa ujumla
iii) Fani ya siasa
Katika fani hii kama serikali itaamua kuitilia mkazo basi inaweza kuzalisha ajira kupitia tasnia ya siasa kwa kupata viongozi wanaoweza kusimamia majukumu vizuri katika taasisi za umma na serikali na kuweza kupata ajira kupitia sekta hiyo
Zipo kada nyingi ambazo serikali ikitilia mkazo zinaweza kuzalisha ajira kwa vijana na kuweza kujiajiri kupitia kada hizo
Serikali inapaswa kuyafanya haya:-
i) Kuandaa mitaala inayoendana na mahitaji ya sasa ya soko la ajira ili kutoa fursa kwa vijana kuanzia ngazi elimu za msingi kuamua khatma ya maisha yao ya baadae kwa kuwaandalia misingi bora ya kujifunzia katika nyanja mbalimbali za elimu kama ufundi stadi,kilimo,siasa na stadi za mazingira
ii) Kuboresha mazingira ya kufundishia kuanzia dhana za kufundishia na dhana za kujifunzia kutokana na kada ya elimu mwanafunzi aliamua kujifunza
iii) Kujenga vyuo vya kati vingi vitakavyo waanda wanafunzi mazingira na namna bora kujiajiri katika fani mbalimbali kama zilivyo veta za sasa na kuongeza kada nyingi katika vyuo hvyo ili kumuwezesha mwanafunzi kuwa na uwanja mpana wa kuchagua stadi ya kazi anayoipenda kujifunza
iv) Kutoa motisha ya mikopo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika kada zao na kuwasimamia katika kuendeleza mitaji yao ya mikopo atika nyanja mbali mbali za ujasiriamali kama ufundi stadi,uvuvi,kilimo ,afya na mazingira
v) Vyuo vya ustadi viwezeshwe katika kuandaa ajira mbadala kwa wanafunzi wanapohitimu mafunzo yao kabla vya kuingia katika soko la kujiajiri ili wapate mafunzo vyema na endelevu na kusimamia kazi za wanafunzi
ILIASA KHAMIS
0656040880
Naombeni kura zenu wadau kama umependa

Upvote
3