BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
MITAGATO AMTUMIA WARAKA ASKOFU, AELEZA JINSI ALIVYOSHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA SIKU 11 PASIPO KUFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMANI
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Nashukuru kushiriki kunipazia sauti uliposikia kuwa nilikuwa nimechukuliwa na Jeshi la Polisi. Mimi ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CHADEMA Kanda ya Magharibi yenye Mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi!
Nilikamatwa siku ya Jumatatu tarehe 9 mchana, nikaambiwa RCO wa Kigoma ana shida na mimi. Nikaondoka nao mpaka Central Police, na kuwekwa lockup bila maelezo yoyote. Kesho yake Jumanne Saa Tisa mchana nikatolewa na kupelekwa nyumbani kwangu kwa ajili ya kupekuliwa. Tulipofika nyumbani, baada ya upekuzi waliondoka na vifaa vya uenezi vya CHADEMA ambavyo ni bendera, t-shirts, skafu, vitabu, openers na keyholders! Tukarudi Central Police.
Baada ya muda nikaingizwa kwenye gari nikiwa nimefungwa pingu na kuondoka nikiwa sijui ninapelekwa wapi, safari iliendelea mpaka Tabora Central Police nikalala hapo. Asubuhi ya Jumatano nikatolewa lockup (ndani) na kufungwa tena pingu nikaingizwa kwenye gari likiwa na watu watano wenye siraha, ambao sio wale niliotoka nao Kigoma. Mpaka hapo, familia yangu haijui niko wapi!
Safari ikaanza kuelekea nisikokujua, mpaka Saa Tano usiku tukafika Kituo cha Polisi Chang'ombe, Dar es Salaam. Nikashushwa na kuingizwa lockup (ndani) mpaka nilipoachiliwa usiku wa Alhamisi tarehe 19. Niliachiliwa usiku ok baada ya Wanaseheria wa CHADEMA kuwafungulia mashtaka Mahakamani viongozi wa Jeshi la Polisi kwa kutushikiria kinyume cha Sheria. Nilituhumiwa eti kwa kuhamasisha maandamano! Masharti ya kuachiwa kwangu na Jeshi la Polisi ni kwamba nikifika Kigoma niende kuripoti kwa RCO. Simu zangu wamebaki nazo Polisi wa Dar es Salaam!
Kupitia kwako Baba Askofu, ninaomba niweze kuwashukuru wote walioshiriki kunipazia sauti pamoja na Wanasheria wetu.
Mitagato Benjamin
Mjumbe wa Kamati Tendaji,
CHADEMA Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma & Katavi)